Home Kimataifa Amir Khan amshambulia mkewe na kumshutumu kutoka na bondia mwenzake, story kamili...

Amir Khan amshambulia mkewe na kumshutumu kutoka na bondia mwenzake, story kamili hii hapa

3187
0
SHARE

Achana na habari ya Wladmir Klistchko kustaafu ndondi lakini gumzo kubwa katika wikiendi hii katika ulimwengu wa masumbwi ni bondia Amir Khan, mkewe Fryal Makhdoom na bondia mwingine wa Uingereza Anthony Joshua.

Amir Khan amemtuhumu Anthony Joshua kwamba anatembea na Makhdoom, huku Khan akisema kwamba Joshua ndio chanzo cha yeye na mkewe huyo kutalakiana suala ambalo Anthony Joshua amesema sio kweli hata kidogo.

Mtafaruku huu ullianzia katika ukurasa wa Twitter wa Khan baada ya Khan kutupa kijembe kwa Anthony na Makhdoom kuwa wawili hao ni wapenzi na kusisitiza hilo hata halimuumizi kichwa hata kidogo.

Amir Khan aliandika mambo mengi huku moja ya tweet akiandika “mwanamke wangu aliniambia anataka kuwa na mwanaume mwingine ambaye ni Anthony Joshua” na baadae akaandika “hata sina wivu na sihitaji kutumiwa picha za mwanaume mwingine”

Khan alienda mbali zaidi na kutuma screen shot ya mawasiliano kati ya mkewe na mtu aliuyesomeka kwa jina la Ghost wakipanga kuonana huku Ghost mwenyewe akidhaniwa ni Joshua lakini baadae Khan alisema yeye na mkewe wameamua kutengana.

Baadaye mke wa Khan aliibuka naye mtandaoni akimshambulia mumewe kwa kusema kwamba “hakukuwa na haja ya kupost tweet za kijinga vile” huku akidai Khan amekwisha kimasumbwi na hivyo anataka watu wamkumbuke ndio maana akafanya hivyo.

Baada ya mke wa Khan kusema account ya Khan ilihakiwa, mshambuliaji huyo aliibuka tena kupitia mtandao wa Snap Chat na kusema kupitia video kwamba maneno yote aliyosema kuhusiana na mke wake yalikuwa ni ya kweli.

Kwa upande wa Anthony Joshua naye aliibuka kupitia mtandao wa Twitter na kukanusha madai ya Amir Khan akisema “sio mimi”. Taarifa toka mjini Dubai zinasema Fryal Makhdoom amekuwa akijaribu sana kurudisha mahusiano yake na Khan lakini Khan amesema hawezi rudiana na Makhdoom.

Wakati Khan na Makhdoom wakiwa katika mvutano huo kumeibuka model mwingine nchini Ufaransa aitwaye Flore Aguilar ambaye alishawahi kuwa mpenzi wa Mario Balotelli na Ashley Cole ameibuka na kusema alishawahi kulala na Khan wakati akiwa kwenye ndoa.

Amir Khan tayari yuko njiani kuelekea nchini Marekani baada ya kuisha kwa wikiendi iliyokuwa ndefu kwake na sasa amesisitiza kwamba akili yake yote anaielekeza kwenye kipaji chake na mazoezi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here