Home Kimataifa Bayern waibuka kidedea Super Cup

Bayern waibuka kidedea Super Cup

5181
0
SHARE

Klabu ya Bayern Munchen ya nchini Ujerumani imeibuka kidedea katika fainali ya ya Super Cup baada ya kuwafunga wapinzani wao Borussia Dortmund katika mchezo ulopigwa nchini Ujerumani.

Katika fainali hiyo iliyokuwa ya piga nikupige alianza Christian Purisic dakika ya 12 kuifungia BvB kabla ya Roberto Lewandoski kuisawazishia Bayern kisha Emerik Aubamyenag alifunga lingine kwa Bvb na Roman Burki akajifunga.

Baadaye muamuzi wa mpambano huo aliamuru mchezo huo uende katika hatua za penati ambapo golikipa wa Bayern alicheza penati mbili na kuifanya Bayern kuibuka kidedea katika mchezo huo wa Super Cup kwa ushindi wa penati 5 kwa 4.

Lakini pia kulikuwa na michezo mingine ya kirafiki hapo jana ya kirafiki ambapo Liverpool waliifunga 3 Atl Bilbao huku mabao ya Liva yakifungwa na Roberto Firminho, David Solanke na Ben Woodburn.

Tottenham walikuwa uwanjani zidi ya Juventus na kuibuka na ushindi wa maba 2 kwa 0 mabao ya Tottenham yakiwekwa kimiani na Harry Kane na Christian Erikssen.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here