Home Kimataifa Hizi ni takwimu 6 muhimu kuelekea Arsenal na Chelsea lakini mimi leo...

Hizi ni takwimu 6 muhimu kuelekea Arsenal na Chelsea lakini mimi leo karata yangu naiweka timu hii

13169
0
SHARE

Arsenal wanaenda kukutana na Chselse katika mchezo wa ngao ya jamii wakiwa na kumbukumbu ya kuwachapa katika mchezo huo mwaka 2015 huku wakiwafunga tena Chelsea fainali ya FA msimu uliopita, kwa takwimu hizi 6 inawezekana Gunners wakaendelea kuinyuka Chelsea?

1.Timu ya mwisho kuchukua Ngao ya Hisani na kwenda katika msimu wa Epl na kubeba kombe ilikuwa ni Manchester United na walifanya hivyo mwaka 2010.

2.Katika mechi 3 za ngao ya hisani zilizopita Chelsea wamefungwa zote, walifungwa 2010 na Manchester United, wakapigwa 2012 na Manchester City na wakapigwa 2015 na Arsenal.

3.Toka uwanja wa Wembley ufanyiwe marekebisho vijana wa Wenger wamepoteza michezo miwili tu huku michezo 8 iliyobaki wakiwa wameshinda yote.

4.Sanchez amecheza michezo 6 katika uwanja mpya wa Wembley na katika michezo hiyo ameshinda yote na kufunga yote kasoro mchezo mmoja tu zidi ya Manchester City ndio hakufunga.

5.Katika michezo 16 ambayo Chelsea wamecheza katika uwanja huu mpya wa Wembley, vijana hao wa darajani wameshinda michezo 10 tu huku 6 iliyobaki wakishindwa kupata matokeo.

6.Katika fainali 3 za mchezo wa ngao ya hisani zilizopita, mshindi wa mechi hiyo amekuwa ni bingwa wa FA, yaani bingwa wa FA ndiye ambaye amemfunga bingwa wa ligi katika mechi 3 za ngao ya hisani zilizopita.

Achana na hizo takwimu kwakua mpira ni dakika 90 na sio historia lakini kwa Arsenal walivyo naona wako sawa zaidi kuliko Chelsea wanaoonekana kama kustrugle kutafuta fomu yao waliyomaliza nayo msimu uliopita.

Kukosekana kwa Diego Costa na Hazard ambao walikuwa key players msimu uliopita inanipa asilimia nyingi kuamini huenda Guners wakafanya kile walichofanya mwaka 2015 katika mechi hii na kuendeleza utemi kwa Chelsea katika ngao ya hisani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here