Home Kitaifa Yanga wamethibitisha Gadiel Michael amesaini mkataba, Azam wamewapa sharti gani?

Yanga wamethibitisha Gadiel Michael amesaini mkataba, Azam wamewapa sharti gani?

23179
0
SHARE

Siku za hivi karibuni kumeibuka mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari baada ya beki wa kushoto wa klabu ya Azam Gadiel Michael kulalamika kwamba klabu yake haitaki kumuachia ajiunge na Yanga.

Katbu Mkuu wa Yanga amekiri ni kweli wamemsainisha mkataba Gadiel kujiunga na timu yao lakini mambo hayajaenda kama walivyotarajia baada ya klabu yake kuibuka na kusema mchezaji huyo bado anamkataba ambao ni muda mrefu (mkataba wa Gadiel na Azam utamalizika Disemba 2017) tofauti na wao walivyokuwa wanafahamu kabla.

“Tumemsainisha kweli na mkataba wake upo lakini wao wanatuambia hawawezi kumwachia hadi tulipe (Mkwasa alisema hawezi kutaja ni kiasi gani) lakini ni pesa nyingi sisi hatuwezi kulipa, kutokana na muda wake uliobaki Azam,”Charles  Boniface Mkwasa Katbu Mkuu Yanga.

“Taarifa tuliizopewa awali ni kwamba mchezaji  anamaliza mkataba wake mapema sana lakini baada ya kufanya maandishi na kusaini nae tukakuta kwamba tunaambiwa mkataba wake upo mpaka Disemba, tukajaribu kufanya mawasiliano na wenzetu tuone kama wataweza kutusaidia.”

“Tumeletewa barua ambayo ina siku mbili sasa hivi ya kutupa ada ya kulipa, tunajaribu kuiangalia hiyo ada tunaona kwamba ni kiasi kikubwa sana kiasi kwamba tunaona bora tusubiri hiyo miezi iliyobaki amalize ili tufanye taratibu za uhamisho wake.”

“Tunashangaa mchezaji anapotoka Azam kuja kwetu inakuwa ni kikwazo kuliko mchezaji akitoka Azam kwenda Simba. Simba imesajili wachezaji karibu wanne lakini huwezi kusikia vikwazo kama hivyo lakini kuja Yanga inakuwa ni tatizo.”

Mkwasa pia ametangaza rasmi klabu ya Yanga kuachana na kiungo raia wa Zambia Justine Zulu maarufu kama ‘Mkata umeme’ baada ya kutoridhishwa na uwezo wake uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here