Home Dauda TV Ufafanuzi kuhusu afya ya mshambuliaji wa Ruvu Shooting, klabu tatu za nje...

Ufafanuzi kuhusu afya ya mshambuliaji wa Ruvu Shooting, klabu tatu za nje zinamtaka

5350
0
SHARE

Afisa habari wa Ruvu Shooting Masao Bwire ametoa taarifa rasmi kwamba, kuna klabu tatu za mataifa tofauti zinamuhutaji mshambuliaji wao Abdulrahman Musa ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa na magoli 14 sawa na Simon Msuva na wawili hao kutwaa tuzo ya ufungaji bora wa msimu 2016/2017.

Jambo la pili ambalo Bwire amelizungumza ni utata uliopo kuhusu Musa kutemwa kwenye kikosi cha Stars kwa madai kwamba ni mgonjwa, Bwire amethibisha kwamba Musa yuko fiti na hakuwahi kupimwa na daktari wa Stars na kukutwa ana tatizo.

Mjadala wa Musa kutoitwa Stars ulikuja baada ya kocha wa timu hiyo kumuita John Bocco kuongeza nguvu kwenye kikosi baada ya Mbaraka Yusuph kuumia wakati timu ikiwa Afrika Kusini inashiriki mashindano ya COSAFA 2017.

Bwire amesema Musa hajawahi kuwa na tatizo ambalo limeelezwa na daktari wa Stars, kwa sasa yupo kambini Zanzibar na timu ya jeshi wakijiandaa kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya majeshi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here