Home Dauda TV Sports Pesa waifanya Everton isiisahau nchi ya Tanzania

Sports Pesa waifanya Everton isiisahau nchi ya Tanzania

7319
0
SHARE

Kampuni ya Sports Pesa iliileta klabu ya Everton nchini Tanzania katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza, wakiwa hapa Everton walicheza mchezo wa kirafiki zidi ya mabingwa wa kombe la Sports Pesa klabu ya Gormahia.

Kabla ya siku ya mchezo huo kampuni ya Sports Pesa iliwatembeza baadhi ya wawakilishi wa klabu ya Everton akiwemo balozi wao Leon Osmane sehemu mbalimbali nchini yetu ya Tanzania.

Leon Osmane ameelezea mambo mengi kuhusiana na safari hii huku akikumbuka sehemu za kuoneshea mipira mtaani (vibanda umiza) na safari za mbuga za wanyama ikiwemo Manyara, Ngorongoro na Serengeti.

“Nilifanikiwa kucheza ngoma zao na kuona maneo wanayoangalizia soka, ilikuwa safi sana kwani baadae tulifanikiwa kwenda hadi mbuga za wanyama ambako niliona Tembo pamoja na wanyama wengine akiwemo Twiga”

Naye Wayne Rooney ameelezea furaha yake kukutana na tamaduni tofauti nchini Tanzania haswa alivyokutana na kabila la Wamasai huku pia akifunga moja ya bao katika mechi zidi ya mabingwa wa michuano ya Sports Pesa klabu na Everton.

Hii hapa chini video ya safari hiyo nchini Tanzania kwa ufupi, lakini utaweza kushuhudia mambo mbalimbali waliyofanya wachezaji wakati walipokuwa Tanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here