Home Kitaifa Picha: Haji Manara alivyoiwakilisha Yanga

Picha: Haji Manara alivyoiwakilisha Yanga

8122
0
SHARE

Msemaji wa Simba Haji Manara leo August 3, 2017 aliibuka na kwenda kuwa mwakilishi wa watani wao wa jadi Yanga wakati Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wa ligi kuu Tanzania bara walipokuwa wakigawa vifaa kwa timu 16 zitakazo shiriki VPL 2017/2018.

Manara ambaye alikuwa anaiwakilisha Simba katika zoezi hilo, alisimama kwenda kuiwakilisha klabu ya Yanga baada ya mabingwa hao kukosa mwakilishi.

Models waliovalia jezi za Yanga (nyumbani na ugenini) zitakazotumiwa msimu ujao walipanda kwenye stage lakini alipoitwa mwakilishi kutoka Yanga hakuwepo ndipo Manara akaenda jukwani kuwawakilisha watoto wa Jangwani.

Ikumbukwe vilabu vya Simba na Yanga ni mahasimu uwanjani lakini nje ya uwanja mashabiki wa vilabu hivi ni watani na wamekuwa wakitaniana kwa mambo mengi kitu kinacho tia chachu pindi timu hizi zinapokutana uwanjani.

Siku za hivi karibuni maafisa habari wa vilabu hivi (Haji Manara-Simba na Jeri Muro kabla hajaondoka Yanga) waliongeza hamasa nje ya uwanja kutokana na tambo na matamko yao juu ya timu zao na wakati mwingine wapinzani wao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here