Home Dauda TV Simba Week itakavyogusa mashabiki moja kwa moja

Simba Week itakavyogusa mashabiki moja kwa moja

6184
0
SHARE

Klabu ya Simba imejiwekea utaratibu wa kusherekea siku ya Simba ‘Simba Day’ August 8 kila mwaka, leo Jumanne August 1, 2017 klabu hiyo imezindua rasmi Simba Week kuelekea kilele cha Simba Day ifikapo tarehe 8 August mwaka huu.

Kuelekea Simu hiyo, Afisa habari wa Simba Haji Manara na Imani Kajula ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri wa kibiasha wa Simba kwa pamoja wamezindua Simba Week mbele ya waandishi wa habari na kuanisha mambo muhimu yatakayofanyika katika wiki nzima kuanzia leo hasi siku ya August 8 ambayo ndio itakuwa kilele cha Simba Day.

Baadhi ya mambo yatakayofanywa katika kipindi cha Simba Week ni pamoja na kutembelea watoto yatima, kutembelea watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo, kugawa mipira kwenye kliniki na mengine mengi.

Siku ya yenyewe ya Simba Day klabu ya Simba itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda lakini kabla ya mchezo huo kutakuwa na mechi za utangulizi zitakazowahusisha wachezaji wa zamani vs viongozi wa sasa wa Simba, Simba Queens watacheza pia lakini wapinzani wao watatangazwa kadiri siku zinavyosonga mbele.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here