Home Kimataifa Habari njema kwa mlio single “kampuni ya kutafuta wachumba kuingia mkataba na...

Habari njema kwa mlio single “kampuni ya kutafuta wachumba kuingia mkataba na Manchester United”

8908
0
SHARE

Tinder ni kampuni maarufu sana duniani haswa haswa barani Ulaya, Tinder huwa ina application na watumiaji zaidi ya 50m wanaitumia app hiyo kwa kazi maalum ya kutafuta wachumba.

Katika kuendeleza kujitanua kibiashara kampuni hiyo imeamua kuingia katika soka la Uingereza na kwa kuanza wanaanza na Manchester United ambao sasa watakuwa wakivaa jezi zenye nembo yao.

Hio haitapunguza hata kitu kimoja kwenye jezi ya Manchester kwani logo zote zitakuwepo ikiwemo ya Premier League mkono wa kushoto na Tinder itakaa katika mkono wa kulia.

Kampuni ya Chervolet bado watabaki kuwa wadhamini wakuu wa jezi ya timu hiyo na udhamini mnono wa £50m na hii itawafanya Tinder kutoa 10% ya kiasi kinachotolewa na Chervolet ili nao wawepo kama sehemu ya nembo ya United.

Hii ni mbinu ya Tinder kutafuta wateja wapya ambapo wana ushirikiano pia na klabu ya Napili na mshambuliaji wao Arkadiusz Milik ni kati ya watu maarufu wanaotafutiwa wachumba na Tinder.

Hii inamaanisha mkataba na Manchester United ukianza pia kutakuwa na uwezekano kwa wachezaji kama Paul Pogba, Romelu Lukaku kupewa nafasi maalum kupata wachumba kupitia mtandao wa Tinder.

Taarifa kuhusu Manchester United na Tinder zimezagaa sana lakini msemaji wa klabu hiyo amegoma kuongelea lolote kuhusu mkataba huo kati ya pande hizo mbili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here