Home Kimataifa Kesi ya madawa yaliyokatazwa michezoni yaiumiza Manchester United

Kesi ya madawa yaliyokatazwa michezoni yaiumiza Manchester United

11216
0
SHARE

Shirikisho la soka duniani FIFA linapinga utumiaji wa madawa ya kusisimua mwili kwa wanasoka na huwa linaunda kamati maalum kwa ajili ya uchunguzi wa masuala kama hayo.

UEFA ambao ni wanachama wa FIFA wana sheria ambazo zinawabana wana michezo wa bara la Ulaya kutumia/kuzuia matumizi ya madawa hayo UEFA ANTI-DOPING REGULATION (ADR).

UEFA kupitia sheria zao hizo wameweka kipengele kwamba wachezaji wote ndani ya UEFA ni lazima kufanyiwa vipimo ili kuona kama wanatumia madawa hayo au hapana, vipimo ambavyo huchukuliwa mara kwa mara.

Wakati wa mchezo wa fainali ya michuano ya Europa kati ya Manchester United na klabu ya Ajax kulitokea hali ya kutokeelewana kati ya maofisa wa UEFA waliokuwa wanawapima wachezaji kuhusu matumizi hayo na baadhi ya wachezaji wa Manchester United.

Phill Jones aliingia matatani katika suala hilo kwani alimtolea lugha chafu ofisa mmoja wa tume hiyo na inadaiwa kwamba mlinzi huyo pia alionesha ushirikiano dhaifu sana kwa maofisa wa tume hiyo.

Dalley Blind naye kama ilivyo kwa Phill Jones naye alionesha ushirikiano dhaifu kwa maofisa hao na hakuwa ana ushirikiano wa kutosha huku akijua ilikuwa wajibu wake kuwaoa ushirikiano maofisa hao.

Baada ya kupitia kesi zote hizo mbili UEFA wameamua kumfungia Jones michezo miwili inayoandaliwa na chama hicho na pia kulipa faini ya £5000, huku Dalley Blind naye akipewa adhabu ya kulipa faini ya £5000.

Hii inamfanya Jones kuungana na Eric Bailly jukwaani wakati wa mchezo wa Super Cup zidi ya Real Madrid wote wakitumimia adhabu za UEFA, United wanaweza kukata rufaa kuhusu kesi hiyo ndani ya siku 60.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here