Home Kimataifa Harry Kane amkana Antonio Conte

Harry Kane amkana Antonio Conte

6716
0
SHARE

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amekaririwa akisema kama angepewa nafasi ya kumsajili mshambuliaji mmoja tu baasi angeenda Tottenham kumng’oa mshambuliaji wa timu hiyo Harry Kane.

Kauli ya Conte ilileta gumzo mtandaoni haswa kwa kipindi hiki ambacho Conte amemnunua Morata na wengi wamekuwa wakijiuliza kwamba pengine huenda Conte anamtamani Kane zaidi kuliko Morata.

Chelsea walishawahi kutajwa kujaribu kumnunua Harry Kane ambaye thamani yake inatajwa kuwa £100m kwa muda lakini Tottenham wamekuwa imara kuzuia wachezaji wao wote mahiri kuondoka katika klabu hiyo.

Kane ameyasikia maneno ya Antonio Conte na ameshukuru kwa kocha huyo kumkubali lakini akasisitiza ana furaha kubwa sana kuitumimia Tottenham na kwa sasa hana mpango wa kwenda popote.

“Ni maneno mazuri aliyosema lakini mimi kwa sasa naiwaza Tottenham tu na kile ambacho kocha wangu ananiambia,nawaza nini napaswa kufanya na kujiandaa na msimu mpya wa ligi” alisema Harry Kane.

Kane alikuwa na msimu mzuri sana uliopita akiisaidia Tottenham kumaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku yeye akiibuka kinara wa ufungaji nchini Uingereza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here