Home Dauda TV Video: Mashabiki wa Misosi walivyopika na kula ugali kwenye uwanja wa Ndondo

Video: Mashabiki wa Misosi walivyopika na kula ugali kwenye uwanja wa Ndondo

4952
0
SHARE

Hakika michuano ya Ndondo ni ya aina yake na mambo yake hayapatikani kwingine zaidi ya kwenye michuano hii, burudani ndani na nje ya uwanja. mashabiki wanaojitoa kweli kwa ajili ya timu zao wapo huku.

Kilichotokea kwenye mchezo wa robo fainali ya tatu ya michuano hii ni mashabiki wa Misosi FC kuamua kulibeba jina la timu yao ‘Misosi’ kwa kupika ugali na mboga uwanjani kisha kula.

Jamaa walikuja na vifaa vyote (majiko mawili moja la mkaa jingine la gesi, unga, maji, mboga na miko) wakati game inaendelea kati ya Misosi na Mpakani Kombaini, wao wakawa wanafanya yao nje ya uwanja.

Baada ya ugali kuiva ukaliwa palepale  uwanjani huku mashabiki hao wakiwa na furaha ya ushindi wa 3-0 iliopata timu yao ya Misosi FC dhidi ya Mpakani Kombaini na kukata tiketi ya kucheza nusu fainali ya Ndondo Cup 2017.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here