Home Kimataifa Jose Mourinho akosa imani na wamiliki wa Manchester United

Jose Mourinho akosa imani na wamiliki wa Manchester United

13834
0
SHARE

Dirisha la usajili linaendelea tu huku nchini Uingereza Manchester City wanaonekana kutembeza pesa sokoni na kuchukua yoyote wanayemtaka ili kuimalisha kikosi chao.

Manchester United hadi hivi sasa wamesajili wachezaji wawili tu lakini tetesi kuhusu usajili wao zimekuwa ni nyingi sana kuliko usajili wenyewe jinsi unavyokwenda.

Baada ya kumnunua Lindelof na Romelu Lukaku kulikuwa na taarifa kwamba Nemanja Matic na Ivan Perisic wako njiani kuelekea Old Traford na wakati wowote dili hizo zinaweza kukamilika.

Jose Mourinho alithibitisha kwamba United wanahitaji wachezaji wawili wengine haswa winga na kiungo mkabaji lakini hadi hivi sasa hakuna kinachoendelea.

Taarifa zinasema United wameshindwana na Inter kuhusu Perisic baada ya United kugoma kutoa £48m na pia hawataki kutoa £40m kwa Nemanja Matic na usajili wa Eric Dier nao unaonekana umeota mbawa.

Jose Mourinho amekosa furaha kutokana na hali ya usajili ndani ya klabu hiyo inavyoendelea na anaona familia ya Glazer na mkurugenzi Ed Woodward wanachukulia poa suala la kuleta wachezaji wapya.

Mourinho anakosa raha kwani hadi hivi sasa usjili aliopendekeza umekamilika kwa 50% tu huku 50% zilizobaki zinaonekana kama zimeota mbawa, hii leo United watakuwa uwanjani katika mchezo wa kirafiki zidi ya Vaaleranga ya nchini Norway.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here