Home Kimataifa Habari za usajili barani Ulaya hii leo

Habari za usajili barani Ulaya hii leo

8503
0
SHARE

Inasemekana mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Neymar ameiomba klabu ya PSG kumnunua Coutinho, Neymar ambaye yuko njiani kuelekea PSG inasemekana anaaamini muunganiko wake na Coutinho utakuwa hatari.

Wakati huo huo kiungo huyo wa Liverpool Phellipe Coutinho inadaiwa kwamba ameshafanya makubaliano binafsi na klabu ya Barcelona na kinachosubiliwa ni Liverpool kukubali ofa ya Barca.

Klabu ya Liverpool inaonekana iko tayari kumuuza Emre Can kwenda Juventus ambapo klabu hiyo imeshakubali kitita cha £30m kutoka kwa miamba hiyo ya nchini Italia.

Kocha Jose Mourinho ameuthibitishia ulimwengu kwamba bado anahitaji kusajili na safari hii anataka kununua kiungo mkabaji na mshambuliaji ambae atacheza kutokea pembeni ya uwanja

Carlo Anceloti amethibitisha kwamba Renato Sanchez anaweza kuondoka Bayern Munich na kusema kwamba anaweza kwenda kukipiga Epl ambako Manchester United wamekuwa wakitajwa kumnyatia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here