Home Kimataifa Gundogan amsifu Gurdiola huku akiihofia Manchester United

Gundogan amsifu Gurdiola huku akiihofia Manchester United

6513
0
SHARE

Ilkey Gundogan amekuwa na msimu mbaya ndani ya Manchester City kwani tangu alipojiunga nao amekuwa akiandamwa sana na majeraha ambayo yamemfanya kuichezea City michezo 15 tu hadi sasa.

Usajili wa Gundogan toka Borussia Dortmund uliwapa imani mashabiki wa City kubeba kombe lolote lakini hata hivyo msimh uliopita Man City walitoka kapa kwani hawakufanikiwa kubeba kombe lolote.

Gundogan anaamini Man City walipitia wakati mgumu kwani baadhi ya wachezaji wao walikuwa wapya na aina ya uchezaji ambao anautaka Gurdiola ulikuwa mgumu kwao na ndio maana City wakapata tabu.

“Ukiangalia tulifanikiwa kumiliki sana mpira na 95% ya michezo yetu tulikuwa bora sana,kuzoea mifumo ya makocha sio rahisi lakini sasa tuko vizuri na tunaaminibkwa usajili tuliofanya tunaweza fanya vizuri” alisema Gundogan.

“Ukiangalia tulivyocheza unaweza kuona mpura haukuwa fair sana kwa upande wetu, makosa yalikuwepo lakini yalikuwa makosa madogo madogo na sehemu chache za kuzifanyia kazi ikiwemo eneo la ulinzi” 

Lakini kuhusu upinzani wa ligi Ikey Gundogan amesema anaamini majirani zao wa Manchester United wako vizuri zaidi ya msimu uliopita na anaona kama wanaweza kuwapa changamoto kubwa katika mbio za ubingwa.

“United wana timu nzuri na inajengwa na vijana, ukiangalia usajili wa Lukaku umewafanya kuwa imara zaidi ya msimu uliopita,hata Chelsea wamenunua wachezaji na Liverpool bado wanaonekana wagumu kuwakabili” alimalizia Gundogan.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here