Home Kimataifa Gerrad Pique athibitisha kuwa Neymar anaweza kwenda PSG

Gerrad Pique athibitisha kuwa Neymar anaweza kwenda PSG

5231
0
SHARE

Neymar ndio jina linalozungumziwa sana katika usajili hivi sasa, Mbrazil huyo anahusishwa na kwenda PSG na taarifa mbalimbali zinasema kuna uwezekano mkubwa sana wa jambo hilo kutokea hivi karibuni.

Beki wa kati wa Barcelona Gerrad Pique majuzi alionesha Neymar anaweza kubaki baada ya kuandika “anabaki” katika ukurasa wake wa Instagram lakini hata hivyo Pique amesema Neymar hajasema hivyo ila yeye anaamini hivyo.

Gerrad Pique amekiri kwamba kwa sasa ni kweli kuna klabu inajaribu kumshawishi Neymar aondoke ambayo ni PSG lakini yeye pamoja na wachezaji wengine wa Barcelona wanatamani Neymar abaki.

Pique anasema wao kama marafiki wamejaribu kumuambia umuhimu wa kubaki Nou Camp lakini yeye ndio ana maamuzi ya mwisho kama ataondoka au laa japokuwa Pique haamini kama PSG ni mahala sahihi kwa Neymar.

 

“Nadhani hili suala lipo kifedha lakini sio kisoka kwa sababu kama ni kuhusu soka hapa alipo ndio sehemu sahihi kwake ukizingatia kwqmba bado ana miaka 25 tu na hapa yuko na mchezaji bora duniani Lioneil Messi”alisema Pique.

“Kutokana na umri wake kama akienda PSG na wasichukue kombe la Champions League watu hawatampa heshima kubwq na ligi ya Ufaransa sio ligi imara sana kama hii, najua bado anasita kufanya maamuzi lakini sisi tunamshauri zaidi.

Naye mlinzi wa Barcelona Javier Marcherano amekazia kuhusu maneno ya Pique na kusisitiza kwamba wao kama Barcelona Neymar bado wanamuhitaji sana na wasingependa kumuona akienda popote.

“Alichosema Pique ni kweli, hizo ndio hisia za kila mmoja wetu na kila mtu amejaribu kuongea naye ikiwemo Messi,tumejaribu kukaa naye na kumuambia umuhimu wake kwetu kama mchezaji na kama rafiki” alisema Marcherano.

Inasemekana picha ya Pique akiwa na Neymar alioandika kuwa Neymar anabaki ilimkera sana baba yake Neymar pamoja na kaka yake ambao wanajaribu kufanya haraka ili Neymar ahamie katika klabu ya PSG.

Taarifa zinadai tayari Neymar ameshafanya makubaliano binfsi na PSG lakini baadaye ameanza kubadilika na kuwa mgumu kuhusu kumwaga wino PSG ambao wako tayari kuwapa Barca £220m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here