Home Kimataifa Baada ya Morata kwenda darajani, tegemea pengo lake kuzibwa na mmoja kati...

Baada ya Morata kwenda darajani, tegemea pengo lake kuzibwa na mmoja kati ya hawa

13693
0
SHARE

Na Salym Juma, Arusha

Real Madrid ni klabu tajiri yenye mashabiki wengi kila kona ya Dunia. kuna jarida moja liliwahi kuripoti kuwa ‘Pitch’ ya Real Madrid ina thamani kubwa kwani unaweza kuwa mfanyakazi wa ndani wa klabu ya Real Madrid hata kwa miaka 10 na usiikanyage ‘Pitch’ hiyo. Thamani ya Madrid imejengwa na mafanikio iliyopata timu hii sambamba na wachezaji wakubwa waliowahi kucheza Bernabeu. Wachezaji wengi wamekuwa radhi kukaa kwenye benchi la Madrid na sio kuhama.

Baada ya kuondoka mshambuliaji Alvaro Morata aliyekuwa anakipiga Real Madrid na kutimkia Chelsea, Real Madrid imejikuta ikibaki bila ya mshambuliaji zaidi ya Kareem Benzema. Cristiano Ronaldo mara kadhaa amekuwa akicheza kama namba 9 kutokana na uwezo wake wa kukimbia kupungua ila bado Madrid kwasasa haina namba 9 wa uhakika zaidi ya Kareem Benzema. Japo Bale na Ronaldo wanaweza kucheza namba hii ila mrithi wa Morata bado anahitajika pale Bernabeu.

Kutokana na hili wachambuzi mbalimbali wamekuwa wakitaja baadhi ya wachezaji ambao huenda mmoja wao akarithi nafasi ya Alvaro Morata. Hapa chini ni baadhi ya majina yanayopendekezwa na wengi kabla ya dirisha kufungwa.

Kylian Mbappe ni Mshambuliaji hatari anayekipiga AS Monaco ya nchini Ufaransa. Mbappe amekuwa akitajwa mara kadhaa kujiunga na Madrid kwa ada ya kuvunja rekodi ya usajili Duniani. Inawezekana huyu akawa mrithi sahihi kwani umri mdogo alionao Mbappe unaweza kumpa mafanikio pale Madrid. Mbappe ni mshambuliaji mchanga kwani katika michezo 58 aliyoichezea Monaco ameweza kufunga magoli 27. Anaweza kucheza bila presha hata kama akiwa anatokea benchi.

Madrid inahitaji mshambuliaji ambaye hana presha ya kuanza kama ilivyo kwa Morata kwani kwa sasa hakuna mshambuliaji sokoni mwenye kiwango cha kuanza pale Madrid zaidi ya Costa. Mbappe anaweza kumrithi Morata na hii ni kutokana na kutokea Ligue 1, ligi ambayo hata mshambuliaji wa sasa Kareem Benzema katokea. Miaka 18 aliyonayo inatosha kuwa bidhaa nzuri kwa Madrid katika kutafuta mrithi wa Alvaro Morata ambaye alikuwa hapati nafasi ya kuanza.

Lucas Perez ni mshambuliaji wa Arsenal ambaye majaaliwa yake hayajulikani baada ya usajili wa Lacazette pale Emirates. Lucas Perez anaweza kuwa mrithi sahihi wa Morata hasa kutokana na uzoefu wake wa kucheza ligi kuu ya Hispania. Akiwa Deportivo La Coruña kabla ya kuhamia Arsenal, Perez alicheza michezo 36 na kufunga mara 17. Uraia wake unampa nafasi ya kurejea Hispania licha ya umri wake kuwa mkubwa. Kutopata nafasi Arsenal kunawapa Madrid nafasi ya kumsajili.

Timo Werner wa RB Leipzig inayocheza Bundesliga, anaweza kuwa mrithi sahihi wa nafasi hii. Endapo ningekuwa Zidane nisingechelewa hata punde kutuma ofa pale Leipzig. Werner ni chipukizi hatari ambaye amefanya makubwa kwenye michuano ya mabara iliyomalizika kwa timu yake ya Ujerumani kutwaa ubingwa. Miaka 24 aliyokuwa nayo inatosha kumfanya asiwe na presha ya kuanza pale Madrid. Chipukizi huyu anaweza kufunga kwani katika michezo 43 amefunga mara 26.

Diego Costa wa Chelsea anaweza pia kwenda kumrithi Morata japo hatopenda kusubiri nyuma ya Benzema. Maelewano mabovu baina yake na kocha wake yamefanya awe njia panda hasa baada ya kuambiwa hatakiwi na Conte. Japo anatamani kurejea Atletco ila sidhani kama atajiuliza mara mbili endapo Real watatuma ofa Chelsea. Costa ni Mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa zaidi hata ya Alvaro Morata na huenda akaisaidia Madrid endapo akipata nafasi ya kusajiliwa.

Andrea Belotti aliyezaliwa 20 December 1993 anaweza kuwa mshambuliaji wa mwisho kwenye listi hii. Umri wake, klabu anayocheza na kiwango chake haviwezi kumfanya akatae kwenda Madrid kurithi nafasi ya Morata. Belotti hatochukia kusubiri baada ya Benzema na Ronaldo. Mshambuliaji huyu amekuwa akitajwa kuondoka Torino katika dirisha hili na huenda akahamishia makazi yake jijini Madrid kama mambo yatakwenda sawa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here