Home Kimataifa Alvaro Morata apewa “laana” Chelsea

Alvaro Morata apewa “laana” Chelsea

7115
0
SHARE

Katika soka kuna imani mbali mbali, nyingine zinaletwa na mazoea na nyingine zinaletwa na historia, imani hizi hujengeka kwanza kwa mashabiki na baadae huenda kwa wachezaji wenyewe.

Katika klabu ya Chelsea kuna namba ya mkosi, namba ambayo hakuna mchezaji aliyeivaa haswa kutokea nchini Hispania na akafanya vizuri, wachezaji wote waliopewa jezi hiyo waliboronga.

Sahau kuhusu Herman Crespo ambaye alijikongoja na kufunga mabao 13 ambayo kwa nafasi yake pia hayakuwa mabao mengi,Crespo alivaa jezi namba 9 jezi ambayo inaitwa jezi ya laana (Cursed Jersey) ndani ya Chelsea.

Namba 9 imekuwa ikiwasumbua sana nyota wanaojiunga na Chelsea, unamkumbuka Fernando Torres alivyokuwa mwiba Liverpool?lakini alivyokwenda Chelsea kwa ada ya £50m jinsi mambo yalibadilika sana huku mgongoni akipewa namba 9.

Tangu kuja kwa tajiri Roman Abromovich wachezaji karibia wote walionunuliwa na wakapewa namba 9 walibuma,Metaja Kezman mwaka 2004 alitarajiwa kufanya makubwa na mashabiki walikuwa na imani naye kubwa lakini alipopewa jezi hiyo aliishia kufunga mabao 7 tu.

Yupo Radamel Falcao naye mambo yalimuwia magumu akiwa Chelsea na namba hiyo na yalimnyookea alipoivua na kujiunga na Monaco, kiungo Steve Sedwell mwaka 2008 alipewa jezi namba 9 lakini baada ya mechi 25 tu akaondolewa Chelsea.

Kinda la Kibrazil Franco Di Santo mwaka 2008 alitarajiwa kuwa mchezaji mkunwa baadae wa Chelsea baada ya kununuliwa na Philippe Scolari akampa jezi namba 9 lakini mechi 16 tu zilitosha kumtimua Chelsea.

Alvaro Morata amekuja Chelsea naye amevalishwa jezi hii hii ambayo washambuliaji wote hao wameshindwa kung'ara walipoivaa lakini walipoivua viwango vyao vikaanza kupanda taratibu.

Mashabiki wengi wengi wa Chelsea mitandaoni haswa Uingereza wamekuwa wakipinga Morata kupewa jezi namba 9 huku wengi wakitaka Morata apewe jezi anayoivaa Diego Costa namba 10. 

Huwezi kumhukumu Morata kwa kutofunga katika mechi yake ya kwanza lakini baadhi ya mashabiki wenye mioyo midogo wameahaanza kuhofu kwamba huenda laana ya namba 9 inaanza kumtafuna Morata.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here