Home Kitaifa Watangazaji wa Clouds wameweka ahadi nzito kwa timu za Ndondo kuanzaia robo...

Watangazaji wa Clouds wameweka ahadi nzito kwa timu za Ndondo kuanzaia robo fainali

5524
0
SHARE

Msimu huu michuano ya Ndondo Cup imekuwa ya kipekee na mvuto wa aina yake, hii ni kutokana kwamba, watangazaji wa vipindi vya Clouds Media kuzigombea timu za Ndondo baada ya Mlalakuwa Rangers kuchukuliwa na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Picha lilivyoanza

Wadau wa Mlalakuwa Rangers walikuwa wakibeba mabango mbalimbali kuhusu kipindi cha Leo Tena kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzania saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana. Mashabiki hao walikuwa wakibeba mabango yenye segment mbalimbali pamoja na jina la kipindi wakati mwinginge hadi majina ya watangazaji wa kipindi hicho.

Leo Tena wakatimba Ndondo Cup kumwaga pesa

Wenye kipindi (Leo Tena)  salam zikawafikia wakaona isiwe tabu wakaenda uwanjani kuisapoti timu yao (Mlalakuwa Rangers) kuipa hamasa. Mwakilishi kutoka Leo Tena Dahuu akatimba kwenye mechi ya 16 bora ya Mlalakuwa Rangers vs Buguruni United na kuahidi kununua kila goli kwa shilingi 50,0000 ambapo baadae Mlalakuwa Rangers ilishinda 1-0 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.

Taarifa zikawafikia vipindi vingine

Dunia kijiji, habari zikafika mjengoni kuhusu walichofanya Leo Tena kwa Mlalakuwa Rangers, sasa kila kipindi si TV wala radio wote wakaanza kutaka timu ili wazisimamie kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali.

Draw inabidi kuchezeshwa

Haikuwezekana kila kipindi kupewa timu kiholela maana wengine wangenung’unika baada ya timu zao kufanya vibaya na kusema wenzao walipendelewa na kupewa timu imara huku wao wakipewa vibonde. Wakati huohuo kama ingetokea kila kipindi kichague timu basi kuna uwezekano vipindi zaidi ya kimoja wangechagua timu moja hapa ndipo likaja wazo la kuchezesha darw ili haki itendeke kila kipindi kipate timu yake kwa haki.

Draw ikachezeshwa kila kipindi kikapata timu na kuridhika kwa matokeo yaliyotokea, kwa hiyo kila kipindi sasa kina timu yake na tayari kila kipindi kimetanga mipango yake ya ushindi kuhakikisha timu yao inafanya vizuri kwenye hatua zilizobakihadi kuchukua kombe.

Leo tena wenyewe wamebaki na timu yao Mlalakuwa Rangers, kwa hiyo hawakuwepo kwenye draw ya kila kipindi kupata timu yake. XXL wao timu yao ni Keko Furniture, Jahazi wenyewe wameangukia kwa Mpakani Kombaini, Clouds 360 timu yao ni Misosi FC wakati amplifier watakuwa na Vijana Rangers, Kibada One wameangukia kwa Power Breakfast huku Goms United wakitua kwa Shilawadu na Stim Tosha ikienda kwa wazee wa Alasiri.

“Mpira pesa, tumeanza kwenye mechi iliyopita, tulinunua goli moja kwa shilingi 50,000, tumeamua kuongeza dau na tutanunua kila goli kwa shilingi 100,000 kwa magoli yatakayofungwa ndani ya dakika 90. Wakiingia fainali kila goli litanunuliwa kwa shilingi 500,000,” Musa Hussein mwakilishi Leo Tena.

“Keko Furniture tutawapa deals za kutengeneza furniture za wasanii, kila nyumba ya msanii mmoja itahusika kwa kifaa kimoja kama ni coach au shelf ya kutunzia tuzo zao, tutawakutanisha na wasanii wanaowataka,” ahadi ya Adam Mchomvu kwa Keko Furniture, Mchomvu anatoka XXL.

“Mchezaji yeyote atakaefunga goli au atakaetajwa kuwa man of the match tutawapeleka gym ili waendelee kujiweka fit hata mashindano yatakapoisha wawe fit, kila goli litanunuliwa kwa 100,000 na wakifika nusu fainali kila goli 200,000, fainali kila goli 1,000,000,” Gadner Habash Mwakilishi kutoka kipindi cha Jahazi (timu yao ni Mpakani Kombaini).

“Kila goli hatua ya robo fainali shilingi 200,000 timu ikishinda itapata shilingi 500,000,wakichukua kombe la Ndondo Cup timu nzima itaenda kutembelea mbuga ya Serengeti,” Babbie Kabae mwakilishi wa Clouds 360.

“Tutatangaza habari zote za Vijana Rangers hadi mwisho wa mashindano, wakishinda mechi tutawapa ‘vitumbua vya Everton’ maana ndio siri ya ushindi, Everton walivyokuja Tanzania walikula vitumbua wakawafunga Gor Mahia. Sisi kwenye kipindi chetu tunazungumza na watu wa maana, tutawapeleka watu wazito kwenye kila mechi za Vijana Rangers,” Meena Ally mwakilishi wa Amplifier.

“Kila mechi ambayo Goms watacheza tutakuwa tunapeleka star wa kike, na tukiona wapinzani wetu wanatuzidi tutakua tunawatoa mapovu kwa kuzifatilia familia zao” Team Shilawadu Soudy Brown na Qwisar Mzee mkavu.

“Sisi tutawaloga tu kila timu tutakayokutana nayo itapigwa ‘ngindo’ hakuna mchezo ni mwendo wa kuwkaanga hadi kieleweke,” Mbwiga Mbwiguke mwakilishi kutoka Power  Breakfast (timu yao Kibada One).

“Tutakuwa tunafanya dua kila tunapocheza mechi zetu , wakati wengine wakipiga ngindo sisi tutakuwa tunafanya dua kumuomba Mungu atuongoze kwenye mechi zetu,” James Tupatupa mwakilishi wa kipindi cha Alasiri.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here