Home Dauda TV Video: Vita mpya Ndondo Cup 2017, hii ni ratiba nzima ya robo...

Video: Vita mpya Ndondo Cup 2017, hii ni ratiba nzima ya robo fainali

4034
0
SHARE

Usiku wa Julai 24, 2017 zoezi la draw ya Ndondo Cup 2017 hatua ya robo fainali lilikamilishwa na kila timu kujua itacheza na nani katika hatua hiyo itakayoanza kupigwa kuanzia Julai 27, 2017.

Baada ya timu nane kufuzu hatua ya robo fainali kwa kushinda mechi zao za mtoano katika 16 bora, zitapambana kuwania kufuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya Ndondo Cup katika msimu wake wa nne.

Zoezi la draw lulikuwa live kupitia Clouds TV pamoja na Dauda TV (YouTube) vilevile kwenye mitandao ya kijamii ya Ndondo Cup sambamba na ile ya Shaffih Dauda.

Wadau wa Ndondo Cup, viongozi wa timu shiriki, waandishi wa habari na watangazaji wa Clouds Media Group, wote kwa pamoja walishiriki katika draw hiyo iliyofanyika ofisi za Clouds Media maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Hii hapa chini ndio ratiba kamili timu na tarehe za mechi za robo fainali ambapo mechi zote zitachezwa kwenye uwanja wa Kinesi, Shekilango, mtaa wa Victor Wanyama Dar es Salaam.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here