Home Kitaifa Ndoto ya wadau wa Ndondo mikoni imewafikia Mcheza, kaeni mkao wa kula

Ndoto ya wadau wa Ndondo mikoni imewafikia Mcheza, kaeni mkao wa kula

3493
0
SHARE

Ile ndoto ya wadau wengi wa Ndondo Cup kufika mikoani hatimaye imetimia baada ya kampuni ya michezo ya kubashiri ijulikanayo kwa jina la Mcheza kuibeba michuano hiyo mgongoni na kuipeleka mikoa mingine tofauti ukiachana na Dar es Salaam ambapo ndio mashindano yamekuwa yakifanyika kwa mwaka wan ne sasa.

Mwakilishi wa Mcheza Moses Simon amesema walikuwa kimya kwa muda mrefu lakini walikuwa wakijipanga kwa ajili ya mambo mazuri hatimaye mambo yamekaa sawa wameamua kuingia kwenye Ndondo kwa miguu miwili.

“Tulikuwa tunajipanga ili tukiingia tufanye mambo makubwa kama hili la kupeleka Ndondo kwenye mikoa mingine, kwa hiyo hatukutaka kuingia mapema halafu tukawa bado hatuko tayari kufanya vitu vikubwa ambavyo watu wanatarajia. Tunaichukua Ndondo na kuisambaza nchi nzima,”  Moses Simon.

Mbali na kuipeleka Ndondo  kwenye mikoa mingine, Mcheza wanaiongezea thamani michuano hiyo ambapo Simon ameahidi kuongeza pesa nyingi kwa ajili ya kikundi bora cha ushangiliaji ambacho kitatangazwa siku ya fainali ya Ndondo Cup.

“Tutaongeza pesa nyingi (hakutaja kiwango) kwa ajili ya kikundi cha ushangiliaji kitakachoshinda, vikundi vya ushangiliaji vinatoa hamasa kwa wachezaji lakini vinaleta burudani kwa watazamaji wa michuano ya Ndondo kwa hiyo wanastahili kupewa heshima yao ndio maana sisi Mcheza tutatoa zawadi kwa kikundi kitakachotangazwa mshindi.”

Kwa upande mwingine, Mcheza wamedhamiria kufanya makubwa kama walivyosema awali, watawawezesha wachezaji watatu chipukizi (ambao hawajawahi kucheza ligi kuu).

“Tutachukua wachezaji watatu ambao hawana majina kabisa na kuwawezesha, jopo la makocha watatuambia ni wachezaji gani baada ya mashindano.”

Mcheza wataendelea kutoa kiasi cha shilingi 150,000 kwa kila timu itakayoshinda mechi na 100,000 kwa timu iliyofungwa huku mchezaji bora wa kila mechi akivuna shilingi 50,000 kama walivyofanya kuanzania mechi za hatua ya 16 bora.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here