Home Kimataifa Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu ya leo

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumatatu ya leo

9060
0
SHARE

Klabu ya Manchester City imezidi kumwaga pesa baada ya hii leo kufanya usajili wa £52m kumnunua beki wa Monaco Benjamin Mendy ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Man City.

Kwa usajili huo Man City hadi sasa wanakuwa wametumia £306m katika kusajili wqlinzi na golikipa tangu mwaka 2014 na huku msimu huu huyo akiwa beki wa tatu kusajili baada ya Kyle Walker na Danilo.

Virgil Van Dijik ambaye anahitajika katika vilabu vya Liverpool na Chelsea ameachwa katika safari ya klabu ya Southampton kwenda nchini Ufaransa kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

Baada ya kumnunua Alvaro Morata sasa klabu ya Chelsea imehamishia nguvu zake kwa Southampton ambapo wanataka kuwachukua Ryan Bertand na Cedric Soares kwa pamoja.

Lioneil Messi ameiomba klabu yake ya Barcelona kujaribu kumnunua Paulo Dyabala kutoka katika klabu ya Juventus, ikumbukwe Dyabala naye ni Muargentina na ameshaanza kufananishwa ubora wake na Diego Maradona.

Baada ya tetesi kuhusu kuondoka Barcelona kuzagaa, hatimaye Neymar amekutana na Lioneil Messi na Suarez na kuwaambia hana mpango kuondoka Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here