Home Kimataifa Habari kubwa za usajili ndani ya Manchester United

Habari kubwa za usajili ndani ya Manchester United

11754
0
SHARE

Baada ya kumnunua Romelu Lukaku na Lindelof klabu ya Manchester United imeonekana kuwa na matokeo mazuri katika michezo ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu nchini Uingereza.

Lakini Jose Mourinho anaonekana bado ana hamu ya kuongeza wachezaji na haswa anaonekana kutafuta viungo katika eneo la kiungo mshambuliaji.

Ivan Perisic amesafiri na Inter Milan kwenda nchini China lakini kocha wa Inter Millan Luciano Spalleti amesema ni wazi kwamba wanaweza kumuuza Perisic endapo United watafika dau.

Spalleti amesema ingekuwa yeye ndio anamuamulia Perisic angependa abaki Inter lakini Perisic ndio mwenye maamuzi kwa hiyo United wakileta £48m watamuuza.

Lakini wakati huo huo inasemekana United wanaweza kutumia mwanya wa Marco Verrati kuwa chini ya Mino Raiola ili kunasa saini ya kiungo huyo wa PSG.

Raiola amekuwa na uhusiano mzuri na United katika masuala ya kibiashara ambapo amekuwa akiwauzia wachezaji kwa siku za karibuni akiwemo Paul Pogba na Romelu Lukaku.

United wanajaribu kuongea na Raiola kuona jinsi ya kumnunua Verrati ambapo thamani yake inatajwa kuwa ni £70m na Manchester United wako tayari kulipa kiasi hicho.

Lakini ugumu kwenye dili la Verrati umekuja baada ya PSG kutaka Anthony Martial awepo katika sehemu ya dili hilo kitu ambacho United hawako tayari kukifanya.

Wakati huo huo Mourinho amesema kuzungumzia usajili wa Gareth Bale kwenda United ni ujinga kwa kuwa hilo jambo haliwezekani na halipo.

“Iko wazi Bale anapapenda Madrid na anapenda changamoto za pale na yupo katika klabu ambayo ina maendeleo na nzuri, sijawahi kutaka kumsajili hilo halipo” alisema Mourinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here