Home Kitaifa Exclusive: Gadiel Michael amezungumzia tetesi za kuhamia Yanga

Exclusive: Gadiel Michael amezungumzia tetesi za kuhamia Yanga

19711
0
SHARE

Tetesi na mabishano yamezidi kuchukua nafasi kubwa kwenye vijiwe mbalimbali na sehemu nyingine nyingi mitaani watu wakibishana kuhusu beki wa kushoto wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Gadiel Michael wengine wakidai kwamba anaihama klabu yake ya Azam na kujkiunga na mabingwa wa VPL Yanga wakati wapo wanaobisha.

Shaffihdauda.co.tz ikaona ni vyema kumtafuta mwenyewe Gadiel ili azungumzie ukweli kuhusu suala hili na kumaliza utata uliopo, timu ya shaffihdauda.co.tz ikafanikiwa kufanya mahojiano maalum na Gadiel jijini Mwanza ambako alikuwa kambini na timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaochezwa leo Juali 22, 2017 dhidi ya Rwanda kuwania kufuzu fainali za CHAN 2018.

“Hizo taarifa zipo, watu wengi wanasema hivi na vile mara mimi nakwenda Yanga, lakini kwangu mimi siwezi kuliweka wazi hilo kwa sababu bado nina mkataba na Azam, mkataba wangu na Azam utakapomalizika ndio tutajua nabaki Azam au naenda Yanga lakini kwa sasa hivi siwezi kusema chochote kwa sababu bado nina mkataba na Azam na bado nipo Azam,” Gadiel Michael.

“Mkabata wangu na Azam umebakiza miezi miezi mitano (5) (hadi mwezi Disemba) chochote kinaweza kutokea kuanzia hapo lakini kwa sasa siwezi kusema lolote kwa sababu nipo ndani ya mkataba na Azam.”

Kwa sasa Gadiel yupo kwenye kiwango cha juu na amefanikiwa kucheza mechi zote za Stars ambazo Mohamed Hussein hajacheza tangu alivyopata majeraha kwenye fainali ya kombe la Azam Sports Federation Mei 27, 2017 dhidi ya Mbao FC.

Gadiel alifanya vizuri kuanzia mechi ya Stars dhidi ya Lethoto iliyochezwa uwanja wa Azam Complex kabla ya michuano ya COSAFA 2017 nchini Afrika Kusini ambapo alicheza mechi zote na kufanya vyema. Alikuwepo pia kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya kwanza kuwania kufuzu michuano ya CHAN 2018 wakati Stars ilipotoka sare ya goli 1-1 kwenye uwanja CCM Kirumba, Mwanza.

Inaelezwa kwamba, tayari Yanga imeshamalizana na Gadiel huku nyota huyo akisubiri kumaliza mkataba wake na Azam na huenda akajiunga na mabingwa hao wa VPL katika dirisha dogo la usajili. Yanga wanataka Gadiel akasaidiane na Haji Mwinyi katika nafasi ya ulinzi wa kushoto kutokana na klabu hiyo kuachana na Oscar Joshua ambaye mkataba wake umemalizika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here