Home Kimataifa Neymar to PSG: Hivi ndivyo waarabu wanavyoweza kutumia Trillioni 1+ kumsaini

Neymar to PSG: Hivi ndivyo waarabu wanavyoweza kutumia Trillioni 1+ kumsaini

24476
0
SHARE

Sakata la usajili wa mchezaji Neymar kwenda Paris Saint Germain linazidi kushika hatamu.Taarifa mpya zinasema mbinu walizotumia FC Barcelona kumpata Neymar wakati akiwa mchezaji wa Santos ndio huenda zikamuondoa Neymar Camp Nou.

Wakati FC Barcelona walipokuwa wakiwinda saini ya Neymar walilipa kiasi cha 40 million euros kwa baba mzazi wa Neymar kupitia kampuni yake ya DIS. Malipo haya mwanzoni yaliripotiwa kuwa mkopo lakini baadae jambo hili lilipelekea kuwepo kwa kesi mahakamani na ikafahamika haikuwa mkopo, bali kifuta jasho cha kufanikisha mwanae haendi kujiunga na Madrid bali Barcelona- wakati tayari Neymar alikuwa ameshafanya vipimo vya afya na alikuwa akikaribia kujiunga na Real Madrid. Vilabu vyote viwili vilikuwa vimekubali kulipa ada ya uhamisho iliyotakiwa na Santos.

Miaka 3 baadae, akielekea msimu wake wa 4 na FC Barcelona, miamba ya soka ya Ufaransa Paris Saint Germain wanataka kumsaini Neymar kutoka FC Barcelona. Miamba hiyo yenye misuli ya pesa wapo tayari kutumia zaidi ya trillioni 1 za kitanzania kufanikisha uhamisho huo wa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Brazil.

Mwanzoni taarifa hizi zilipoanza kutoka , watu wengi tuliamini PSG wasingeweza kuvunja rekodi ya dunia kwa kulipa kiasi cha £197m ili kumsaini, kwasababu wangekuwa wametoka nje ya sheria ya Financial Fair Play na hata juzi Rais wa Barca, Josep Bartomeu alikaririwa akisema haamini kama kuna klabu itaweza kumsaini Neymar kwa kuvunja mkataba wake kwa maana ya kulipa kiasi hicho cha pesa.

Leo ripoti mpya za usajili wa Neymar zinaeleza kwamba mchezaji huyo kupitia baba yake tayari amekutana na PSG na kukubaliana vipengele binafsi na tayari Neymar ameshawaambia baadhi ya wachezaji wenzake kwamba anaondoka Camp Nou.

Swali PSG watafanikishaje uhamisho huu bila kuvunja sheria ya Financial Fair Play? .

Jibu: Ili PSG waweze kukamilisha uhamisho huo bila kukabiliana na adhabu za Financial Fair Play, wamiliki wa PSG, serikali ya kifalme la QATAR 🇶🇦 wanaripotiwa kumpa Neymar Dos Santos mkataba wa kuitangaza michuano ya kombe la dunia 2022 itakayofanyika nchini humo kwa mkataba wenye thamani ya €222m. Neymar atatumia fedha hizo kulipa fedha za kuuvunja mkataba wake na FC Barcelona wenye thamani sawa na fedha atakazopewa kwenye dili la kuitangaza michuano ya World Cup 2022. Baada ya kukamilisha usajili huo, Neymar anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka wenye thamani ya €150m. PSG pia watatumia kiasi cha €156m kwa ajili ya kodi. Kwahiyo uhamisho huu utagharimu jumla ya €528m – zaidi ya trillioni 1 za kitanzania.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here