Home Kitaifa Maoni ya timu kuhusu maandalizi yao ya ligi na matarajio yao kwa...

Maoni ya timu kuhusu maandalizi yao ya ligi na matarajio yao kwa ujumla

4643
0
SHARE

Jumanne Chale -Kocha msaidizi

Tangu tumeanza maandalizi mazoezi yanakwenda vizuri na mwalimu anafanya kazi yake vizuri mpaka sasa hivi, wachezaji wote wapo vizuri na hatuna majeruhi sana na kila kitu kinakwenda vizuri mpaka sasa hivi.

Kila timu huwa inajiandaa kwa ajili ya kuchukua kombe na sisi kama SIngida tumejipanga kuchukua kombe maana kama unavyoona mazoezi yetu tunafanya kwa siku mara mbili, tunafanya mazoezi kwa nguvu na wachezaji unawaona wapo vizuri na ni wiki ya pili sasa.

Tutahakikisha tunachukua ubingwa ili tuweze kuleta mageuzi ya soka katika nchi hii kwani tumakamilika kila idara.

Nizar Khalfan -Nahodha

Mazoezi ni mazuri tangu tumeanza na mpaka sasa tumeshapata mechi moja ambapo tumeangalia mwenendo wetu wa timu vipi na kwakweli tunaendelea vizuri sana kwani tumanza mazoezi mapema na wachezaji wamezoeana mapema

Timu yetu imebadilika sana tangu tucheze mashindano ya SportPesa Super Cup kwani kipindi kile wachezaji mazoea kulikuwa hamna tofauti na sasa hivi tunacheza vizuri, tunatoa pasi na kila mtu anajua akipiga wapi pasi mwenzake anaweza kuukuta mpira na hicho ndicho kitu kikubwa katika timu.

Tuna malengo makubwa kwa msimu ujao na tunataka kuleta upinzani mkubwa na ikiwezekana tuweze kumaliza katika nafasi tatu za juu kwasababu tumefanya usajili mzuri ambao upo makini na mwalimu ana uzoefu mkubwa katika ligi hii ya Vodacom kwani amekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kwahiyo anazijua timu zote za ligi.

Tuna mwalimu mzuri, tuna kikosi kizuri na tunafanya mazoezi vizuri tupo fiti na uzuri ni kuwa tumeanza mazoezi mapema sana ili wachezaji waweze kuzoeana

Atupele Green

Mwalimu anatupa mazoezi mazuri, tunafanya vile yeye anataka. Timu yetu ni mpya na ina malengo ya kufanya vizuri katika msimu ujao na mwalimu ni mzuri, mazoezi yake ni bora ambayo yanaweza kutufikisha malengo ambayo sisi wenyewe tumeyakusudia

Elisha Muroiwa (Nahodha Msaidizi) (Raia wa Zimbabwe)

Tunaendelea vizuri na mazoezi na nina furaha kwani hatuna majeruhi wengi na hii ni nzuri kwa timu pia kwa tunapata wasaa wa kujuana vyema.

Tunajua ligi itakuwa na changamoto lakini matarajio yetu makubwa ni kushinda kila mechi inayokuja na tuweze kuwania ubingwa na kama mambo yataenda poa basi tunataka kuchukua ubingwa ili tuweze kucheza kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika msimu unaofuata. 

MAONI YA WACHEZAJI KUHUSU MDHAMINI WA TIMU -SPORTPESA

Nizar Khalfan –Nahodha

Kikubwa nawaomba SportPesa wasichoke na hatutaweza kuiachia hii nafasi kwani tumepata udhamini wa mwaka mmoja kwahiyo tunaamini watatuongeza mkataba kutokana na upinzani tutakaouleta kwenye ligi kwasababu tutakuja kufanya kitu kikubwa sana.

Tunajua tuna mkataba wa mwaka mmoja na tunataka kuongeza miaka mingine mbele kwahiyo hatutaweza kuiachia hii nafasi

Wadhamini wanatusaidia sana kwa sasa kwasababu tumepata jezi na vifaa vingine vingi vya mazoezi kwahiyo sisi wachezaji tunatakiwa kupiga kazi, hivyo wao kama wadhamini wana mchango mkubwa kwenye timu.

Atupele Green

Udhamini ni mzuri, unaleta hamasa katika timu na umesaidia benchi la ufundi kuweza kufanya usajili mzuri kwenye timu ili kuleta changamoto katika ligi yetu

Elisha Muroiwa (Nahodha Msaidizi) (Raia wa Zimbabwe)

Tunashukuru kwa kile wanachokifanya kwa timu naudhamini wao unavutia wachezaji wengi wazuri kujiunga na timu yetu husuani pale wanapoona timu ina wadhamini wakubwa kama SportPesa

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here