Home Ligi EPL Kwa sababu hizi ‘piga ua’ jiandaeni kumuita Lacazette mchawi wa magoli pale...

Kwa sababu hizi ‘piga ua’ jiandaeni kumuita Lacazette mchawi wa magoli pale Emirates

15408
0
SHARE

Na Salym Juma, Arusha

Jezi namba 9 ndiyo iliyokabidhiwa kwa mshambuliaji mpya wa Arsenal aliyesaini mkataba  wamiaka 5 mnamo July 5, 2017.

Sitopenda kuizungumzia jezi hii ambayo imekuwa na bahati mbaya kwa wachezaji wa Arsenal siku za karibuni ila natumia nafasi hii kujadili majaaliwa yake pale London. Mchezaji anayezungumziwa hapa ni Alexandre Lacazette, Nyota mpya wa Arsenal aliyeikaribia rekodi ya Juninho ya kuwa Mfungaji bora wa muda wote pale Lyon. Kiwango chake murua misimu kadhaa mfululizo bila kutetereka kimemfanya asajiliwe London.

Kwa misimu mitatu mfululizo, Lacazette amekuwa akifunga zaidi ya magoli 20 akiwa na Olympique Lyon. Kuna maswali mengi sana juu ya usajili wa mchezaji huyu pale London. Wapo wanaoamini huenda akafanya vizuri huku wengine wakiamini Lacazette huenda ‘Aka-flop’. Mawazo yote haya yatajibiwa vizuri msimu utakapoanza ila kimaandishi watu wengi tunaamini mshambuliaji huyu huenda akawa mwiba kutokana na sababu zifuatazo.

Uwepo wa wachezaji wa kiwango cha Dunia wanaomzunguka Lacazette kama Granit Xhaka, Laurent Koscielny na Petr Cech utamfanya ang’ae zaidi ya alivyokuwa Lyon. Pia viungo kama akina Mesut Ozil na Alexis Sanchez utamfanya mshambuliaji huyu azidi kutakata ndani ya 18. Mawinga hatari wa Arsenal kama Theo Walkot au Chamberline watamtafunia sana mfaransa huyu aliyezaliwa miaka 26 iliyopita na kuichezea timu yake ya taifa kuanzia ngazi ya vijana akiwa na miaka 16 hadi 21.

Staili yake ya uchezaji inastahili kumpa mafanikio pale Emirates. Lacazette mwanzoni alikuwa anachezeshwa kama winga pale Lyon kabla ya kuhamia namba 9. Hakuna winga asiyekuwa na mbio hivyo mshambuliaji huyu ana mbio nyingi sana tofauti na baadhi ya washambuliaji ambao ni wazito. Lacazete anatumia miguu yote na hii itakuwa hatari sana kwa wapinzani. Uwezo wake mkubwa wa kukaba na ‘ku-pace’ ulimfanya afananishwe na Ian Wright.

Uwepo wa wachezaji na kocha kutoka Ufaransa ni sababu nyingine inayotarajia kumng’arisha Lacazette. Sababu hii itamfanya aweze kujiamini na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwao pia. Kumbuka hii inaweza kuwa sababu kubwa iliyochangia kukamilisha usajili wake pale Arsenal. Olivier Giroud, Francis Coquelin, Mathieu Debuchy na Laurent Koscielny ni baadhi ya wafaransa ambao wanapata nafasi ya kucheza chini ya Wenger. Hali hii itamfanya kutumia vyema ushirikiano atakaopata nje ya uwanja.

Kipaji chake cha kufunga kinadhihirisha mwendelezo mzuri ndani ya jezi ya Arsenal. mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Arsenal ameweza kufunga goli na hii ni alam kwa mabeki wa EPL 2017-18. Lacazette amecheza michezo 275 na kufunga magoli 129 ikiwa ni wastani wa goli moja kwa kila mechi mbili. Hii ni rekodi bora kwa mshambuliaji wa kiwango cha Dunia kwani rekodi hii haikufikiwa hata na Kareem Benzema aliyecheza Lyon kabla ya kwenda Madrid.

Wimbi la wachezaji waliotoka ligi kuu ya Ufaransa na kufanikiwa pale EPL unazidi kumpa nafasi kubwa ya kufanya vyema. Lacazette anakwenda EPL kukiwa na Wachezaji kama Eden Hazard, Ngolo Kante, Olivier Giroud na Anton Martial ambao wametoka French League 1 na wanafanya vyema na vilabu vyao pale Uingereza. Mbali na uwepo wao pia kuna wimbi kubwa la wachezaji wa kifaransa ambao wamewahi kucheza Arsenal kwa mafanikio akiwemo Thiery Henry.

Kucheza bila presha kutokana na mafanikio aliyoyapata katika umri mdogo ni jambo ambalo linakwenda kumsaidia Alexandre Lacazette. Tofauti ilivyo kwa washambuliaji na wachezaji wengine ambao husajiliwa kwa presha kubwa na mwisho wake hushindwa kufanya vyema, mshambuliaji huyu huenda akacheza bila wasiwasi kwani umri wake na mafanikio yake haviendani ata kidogo hivyo hawezi kuwa na cha kupoteza zaidi ya kuzidi kuboresha na kuongeza rekodi zake.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here