Home Kitaifa Wachezaji wanne waliokamilisha usajili leo Julai 19, 2017

Wachezaji wanne waliokamilisha usajili leo Julai 19, 2017

24705
0
SHARE

Vilabu vya ligi kuu Tanzania bara vinaendelea kukomaa kusajili wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano, hadi sasa inaonekana Simba ndio klabu iliyosajili wachezaji wengi wapya.

Simba imeshasajili wachezaji 10 (Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili, Shomari Kapombe, John Bocco, Emanuel Mseja, Ally Shomari, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Said Mohamed ‘Nduda’, Emanuel Okwi) huku Aishi Manula na Haruna Niyonzima wakitajwa pia kuwa wameshamalizana na Simba.

Simba

Simba imewasaini Erasto Nyoni na Said Mohamed ‘Nduda’ kila mmoja akisaini mkataba wa miaka miwili. Erasto Nyoni amesaini kutoka Azam FC huku golikipa bora wa COSAFA 2017 Nduda yeye akitokea Mtibwa Sugar, wawili hao wote wapo kwenye kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mechi ya marudiano dhidi ya Rwanda Julai 23, 2017 kuwania kufuzu CHAN 2018 Kenya.

Yanga

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wamefanikiwa kumuongeza mkataba wa miaka miwili kiungo wao Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe ambaye alikuwa amemaliza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani.

Singida United

Ingizo jipya kwenye ligi kuu msimu ujao Singida United wamemtambulisha golikipa Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyekuwa akicheza Yanga. Barthez amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo inayofanya usajili wa aina yake msimu huu ukilinganisha na vilabu vingine ambavyo havina majina makubwa nchini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here