Home Dauda TV Video: Majibu ya Erasto Nyoni kuhusu kuondoka Azam FC

Video: Majibu ya Erasto Nyoni kuhusu kuondoka Azam FC

17212
0
SHARE

Baada ya kudumu kwa miaka saba (7) hatimaye Erasto Nyoni ameondoka kwenye kikosi cha Azam FC na kujiunga na Simba akiwa mchezaji huru mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Nyoni mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi kwenye timu amesaini mkataba wa miaka miwili taarifa ambazo zimethibitishwa na wenyewe klabu ya Simba leo Julai 19, 2017.

Shaffihdauda.co.tz na Dauda TV ilifanya mazungumzo na Erasto Nyoni kabla hajasaini mkataba wa kujiunga na Simba kutaka kujua ni kwa nini kumekuwa na wimbi la wachezaji wa Azam kuondoka kwenye klabu hiyo hususan wachezaji ambao wamedumu kwa miaka kadhaa wakiwa na klabu hiyo.

Kama utakumbuka alianza kuondoka John Bocco nahodha ambaye alidumu na Azam kabla na baada ya kupanda kucheza ligi kuu Tanzania bara, akafuatia Aishi Manula (bado haihathibitishwa rasmi), Shomari Kapombe, Hamisi Mcha akaachwa halafu sasa ni Erasto Nyoni.

Nyoni amesema,kabla ya kuitwa kwenye timu ya taifa alienda Azam kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya lakini hawakufikia mwafaka, akaondoka na kuwaacha Azam waamue .

“Azam waliniita kabla hatujaitwa timu ya taifa, tukaongea lakini hatukufikia mwafaka nikaondoka nikawaachia kazi wao kwa hiyo sijui mawazo yao.”

“Katika mpira hivyo vyote vinawezekana, unaweza ukawepo Azam lakini Mungu ndiyo mpangaji wa kila kitu akitaka uendelee sehemu moja utakuwepo lakini riziki yako ikiisha sehemu hiyo basi huwezi kulazimisha,” Erasto Nyoni.

Erasto Nyoni alijiunga na Azam mwaka 2010 akitokea Vital ‘O ya Burundi na ndio mchezaji pekee ambaye amecheza kwa muda mrefu kwenye timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa wachezaji wa sasa. Nyoni amekuwepo Stars tangu mwaka 2006 hadi sasa akiwa amecheza kwa zaidi ya miaka 10.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here