Home Dauda TV Exclusive: “Tegete alienda kufanya majaribio Ulaya, akarudishwa acheze mechi ya Simba na...

Exclusive: “Tegete alienda kufanya majaribio Ulaya, akarudishwa acheze mechi ya Simba na Yanga” – John Tegete

15878
0
SHARE

Tumemnasa mchezaji wa zamani wa soka la Tanzania lakini kwa sasa ni kocha John Tegete ambaye ni baba mzazi wa mchezaji Jerry Tegete wa Mwadui FC ya Shinyanga na aliwahi kuitumikia pia timu ya taifa ‘Taifa Stars’ miaka kasha iliyopita.

Inawezekana kabisa hukuwahi kujua kama Jerry Tegete aliwahi kupata fursa ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Sweden, Dauda TV imeipata exclusive story nzima kwa baba wa nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji wenye magoli mengi katika derby ya Simba na Yanga kwa siku za karibuni.

“Tegete aliwahi kwenda kufanya majaribio Sweden, lakini alirudishwa haraka sana viongozi wake wakasema ametoroshwa ili asicheze mechi ya Yanga na Simba, mwisho kijana ikabidi arudi. Kurudi hapa wamemtelekeza amekwisha, sasa hivi anacheza timu Mwadui,” – John Tegete, baba mzazi wa Jerry Tegete.

Tegete aliachwa na Yanga wakati Hans van der Pluijm akiwa kocha wa timu hiyo, baadae Tegete alijiunga na Mwadui FC chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ lakini siku za karibuni amekuwa hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Mwadui ambacho kwa sasa kipo chini ya kocha Ali Bushiri.

Kuna wakati Tegete alihusishwa kujiunga na Singida United ambayo msimu ujao (2017/2018) itacheza ligi kuu Tanzania bara ikiwa imepanda kutoka ligi daraja la kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here