Home Kitaifa Mlalakua Rangers imeungana na Goms United kucheza robo fainali Ndondo Cup 2017

Mlalakua Rangers imeungana na Goms United kucheza robo fainali Ndondo Cup 2017

2476
0
SHARE

Malalakuwa Rangers imepata ushindi katika mchezo wake wa hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Buguruni United bao 1-0 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainaki ya Ndondo Cup 2017.

Bao pekee katika mechi hiyo limefungwa na Adam Said dakika ya 12 kipindi cha kwanza goli ambalo limeiacha Buguruni United wakisubiri hadi michuano ijayo ya Ndondo Cup 2018.

Mechi ya leo imeshuhudiwa na Dahuu mtangazaji wa kipindi cha Leo tena cha Clouds FM ambae alikuja uwanja wa Kinesi kuisapoti timu ya Mlalakuwa Rangers ambao wamekuwa wana-show love juu ya kipindi hicho kwa kubeba mabango mbalimbali kila timu yao inapocheza wakiwa wanasifia segment mbalimbali za kipindi hicho.

Dahuu aliahidi kununua kila goli litakalofungwa na Mlalakua Rangers kwa shilingi 50000.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here