Home Kimataifa Adebayor: Hivi ndivyo familia yangu ilivyonikosesha dili la Real Madrid

Adebayor: Hivi ndivyo familia yangu ilivyonikosesha dili la Real Madrid

16160
0
SHARE

Emmanuel Adebayor aliitumikia Real Madrid kwa kipindi kifupi mwaka 2011. Lakini hakuendelea kubaki Santiago Bernabeu, pamoja na kumvutia kocha Jose Mourinho, japokuwa mchezaji mwenyewe alikuwa anataka kubaki na Los Blancos. 
Akiongea katika mazungumzo na kituo cha BBC cha Uingereza, Adebayor amefunguka kwamba moja ya sababu zilizopelekea Real Madrid kutoendelea nae ilikuwa ni barua iliyotumwa na ndugu yake wa kiume kwenda kwa maboss wa Bernabeu, ikiwashauri viongozi wa Real kutomsajili nahodha huyo wa Togo. 

Adebayor anasema alifanya kila kitu ili aweze kuendelea kubaki Madrid. 

Nilifanya kila kitu ili niweze kubaki jijini Madrid, lakini kwasababu ya kaka yangu sikuweza kubaki pale kwasababu alituma barua ….. barua rasmi kutoka kwa familia ya Adebayor ikiwaeleza Madrid kwanini hawatakiwi kunisajili. Hii ilichangia sana kuniharibia mipango yangu Santiago Bernabeu,” alieleza  Adebayor, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya  Basakhesir. 

Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal na Tottenham ana uhusiano mbaya sana na familia yake, familia ambayo anasema hata kuzungumza nao ni mara chache sana. 

Anasema familia yake huwa haimtafuti hata kumsalimu pale anapopata majeruhi au matatizo mengine, kipindi pekee wanachowasiliana nae ni wakati wanahitaji msaada wa kifedha tu. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here