Home Kimataifa Wachina wanavyoliamsha dude lilolala – AC Milan

Wachina wanavyoliamsha dude lilolala – AC Milan

15382
0
SHARE

Soka la ushindani linarejea tena Italia – Juventus wamepata changamoto mpya ambayo inakuja katika shape ya ‘mwamba uliolala’ kama AC Milan ambao wapo katika kukifanyia maboresho makubwa klabu yao ili kurudi katika enzi za ushindi katika soka la Italia na ulaya kiujumla.  

Leonardo Bonucci, mmoja wa walinzi bora duniani kwa sasa, ameondoka Juve kwa ada ya uhamisho wa Euro million 40, akitajwa kusaini mkataba wenye thamani ya 7.5m euro kwa mwaka huku akiwa na bonasi zinazofikia kiasi cha €2.5m. 

Usajili wa Bonucci unaifanya idadi ya wachezaji wapya katika kikosi cha AC Milan kufikia 9, baada ya Matteo Musacchio, Frank Kessie, Ricardo Rodríguez, Andre Silva, Fabio Borini, Hakan Calhanoglu, Andrea Conti na Lucas Biglia.

Pia usajili mwingine muhimu waliofanikisha ni kumsainisha mkataba mpya golikipa wao  Gianluigi Donnarumma baada mwanzoni kusea asingesaini mkataba mpya ambao ulikuwa unebakia kipindi cha mwaka mmoja, akitoa sababu kutoona klabu ikijiimarisha.  

Malalamiko ya Donnarumma sasa yamepatiwa suluhisho, hakuna anayeweza kukitolewa malalamiko tena kikosi cha Vincenzo Montella baada ya kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi chao baada ya muda mrefu wa kukosa mafanikio. 

Na sio tu kwamba Bonucci atakuwa nahodha mpya wa Milan msimu ujao, Massimiliano Mirabelli na Marco Fassone sasa wamepewa majukumu ya mkurugenzi wa michezo na mkurugenzi mtendaji wakati Gennaro Gattuso akirudi kuwa kocha wa timu ya AC Milan under 19.

Uwezekezaji huu unatoka wapi? Baada ya miaka kadhaa ya tetesi juu ya umiliki wa klabu wa waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi, hatimaye PM huyo wa zamani wa Itaky akaiuza klabu hiyo kwa kampuni ya  Chinese consortium inayoongozwa Li Yonghong.

Wamiliki wapya wanafananishwa na walivyokuwa akina Berlusconi mara tu walipoinunua klabu hiyo, walifanikisha timu kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa ulaya mara 2 mfululizo (1989, 1990) chini ya mwalimu Marco Van Basten na Ruud Gullit.

Ligi ya Serie A haijawa na mbio za ubingwa kwa muda mrefu, Roma sasa wamemchukua Monchi kuijenga vizuri timu yao, Inter chini ya wamiliki wapya wa kichina nao wanajiimarisha, Napoli wanaendelea na maboresho ya kikosi na sasa Milan wanaliamsha dude. Baada ya utawala wa Juventus wa miaka 6 mfululizo msimu wa 2017/18 tutegemee ligi tamu ya Serie A. 

Mpaka wameshasajili wachezaji 9, na inaelezwa bado hawajamaliza – sasa inawindwa saini ya aidha Pierre-Emerick Aubameyang kwa €70m au Andrea Belotti – usajili ambao utaifanya Milan kuwa wametumia takribani £250m. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here