Home Kimataifa United na Arsenal zatembeza kichapo

United na Arsenal zatembeza kichapo

4685
0
SHARE

Baada ya Chelsea hapo jana jioni kushusha kipigo cha bao 8 kwa 2 dhidi ya Fulham, hii leo alfajiri Manchester United nao walikuwa uwanjani nchini Marekani.

United walikuwa uwanjanj dhidi ya La Galaxy ambapo United walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5 kwa 2 katika mchezo huo wa kujiandaa na ligi.

Makosa ya mabeki wa La Galaxy yaliwazawadia United magoli ya mapema tu kwanj dakika 27 za mwanzo tu United walikuwa na mabao matatu huku Rashford akifunga mara mbili na Fellaini mara moja.

Kipindi cha pili United waliongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Mkhtaryan na Martial huku yale yakufutia machozi ya La Galaxy yakifungwa na Giovani Dos Santos.

Arsenal nao waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Sydney Fc huku mabao ya Arsenal yakifungwa na Aron Ramsey,Olivier Giroud na Mohamed Elneny.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here