Home Kimataifa “Ninataka kuondoka Arsenal” Sanchez

“Ninataka kuondoka Arsenal” Sanchez

4463
0
SHARE

Muda mwingine waungwana wakizungumza hutumia tafsida ili kupunguza ukali wa maneno na nadhani Sanchez ni muungwana kwani amesema anataka kuondoka Arsenal lakini ameongea maneno hayo kwa tafsida.

Sanchez na Arsenal bado hakijaeleweka na nyota huyo hadi sasa hajasaini mkataba mpya huku kocha wake mzee Wenger akisema nyota huyo hana mpango wa kuondoka na inambidi abaki kwa kuwa ana mkataba na timh hiyo.

Sanchez alizisikia taarifa za babu Wenger bila shaka na yeye kaja na lake ambalo ni tofauti na la babu Wenger kwani haihitaji akili ya darasa la saba kujua kwamba Sanchez haitaki tena Arsenal na anataka kuondoka.

“Mimi tayari nimefanya maamuzi lakini kawaida maamuzi ni ya pande mbili kwahiyo bado nawasikiliza wao lakini iko wazi msimu ujao nataka kucheza katika Champions League na kushinda mashindano hato ni ndoto yangu kubwa” alisema Sanchez.

Arsenal hawapo katika mashindano ya Champions League msimu ujao,Arsenal hawajawahi kubeba kombe la Champions League na hawatabiriwi kufanya hivyo katika siku za karibuni.

Hii inamaanisha nini?Manchester City na Bayern Munich wanatajwa kuhitaji sahihi ya Sanchez na wote wapo katika Champions League na pia wote ni vilabu vinavyoonekana vinaweza kubeba kombe hilo, hivyo ni wazi huenda Sanchez anataka kukimbilia huko.

Hili litakuwa pigo kubwa sana kwa Arsenal kwani Sanchez ndio mchezaji anayeongoza kwa kucheka na nyavu ambapo toka Mchile huyo ajiunge nao ameshawafungia mabao 72 akifuatiwa na Giroud mwenye 59.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here