Home Kitaifa Mkurugenzi wa idara ya michezo amepongeza michuano ya Ndondo Cup

Mkurugenzi wa idara ya michezo amepongeza michuano ya Ndondo Cup

2170
0
SHARE

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania Bw. Yusuph Singo Omari amepongeza mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup kwa kusema ni mashindano mazuri yanayotoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

“Ndondo ni mashindano mazuri sana, nimeshuhudia vipaji vizuri mno. Wachezaji wengi niliowaona hapa wanauwezo mkubwa kabisa wa kucheza ligi zetu za Tanzania, watakapokwenda kwenye ligi kubwa wanaendelezwa na kucheza mbali zaidi.”

“Nilichojifunza ni kwamba, sisi kama serikali inatakiwa tujitahidi tuone jinsi gani tunashirikiana na TFF kuyaboresha mashindano haya. Ni mashindano mazuri sana yanayokutanisha timu nyingi sana na kukutanisha vipaji vingi.”

“Ndani ya vipaji hivi tunaweza tukavuna vipaji vingi na kuondoa kiu ya watanzania   ya kushinda kwenye mchezo wa soka.”

“Ndondo ni nzuri, mimi mwenyewe sikuwa nimeshuhudia sana, lakini leo nitakuwa mshabiki wa Ndondo.”

Bw. Singo alikuwa ni mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ndondo Cup hatua ya 16 bora na kupata kushuhudia vipaji kutoka michuano hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here