Home Kitaifa Himid Mao amezungumzia mechi ya marudiano vs Rwanda

Himid Mao amezungumzia mechi ya marudiano vs Rwanda

2852
0
SHARE

Nahodha anaekiongoza kikosi cha Stars kwenye michuano ya CHAN Himid Mao Mkami amesema, wao kama wachezaji watatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye mechi yao ya marudiao dhidi ya Rwanda kuhakikisha wanafuzu CHAN 2018.

Himid amesema anaamini kocha (Salum Mayanga) atakuja na mbinu nyungine kuhakikisha wanashinda mechi yao itakayochezwa Julai 23, 2017 ili kusonga mbele.

“Tukienda kucheza kwao itakuwa game nyingine nadhani mwalimu atakuwa na plan nyingine, lakini kazi sio nyepesi, tunatakiwa kufanya kazi kubwa sana,” – Himid Mao Mkami.

“Tuliruhusu goli mapema kwa hiyo hata game plan yetu ikabadilika kuanzia hapo tukatakiwa kufunga goli la kusawazisha na kutafuta goli la kuongeza. Wakati kama tungekua hatujafungwa, goli moja tulilopata lingeamua gemu.”

Stars ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya jana iliyochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here