Home Kitaifa Goms UTD imekuwa timu ya kwanza kufuzu robo fainali Ndondo Cup 2017

Goms UTD imekuwa timu ya kwanza kufuzu robo fainali Ndondo Cup 2017

4397
0
SHARE

Michuano ya Sports Extra Ndondo Cup imeendelea leo Julai 16, 2017 ikiwa ni hatua ya 16 bora (mtoano) ambapo kulikuwa na mchezo mmoja uliochezwa kwenye uwanja wa Kinesi kati ya Burudani FC vs Goms United (Temeke Mikoroshini vs Gongo la Mboto).

Goms United imefakiwa kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya Ndondo Cup 2017 baada ya kuifunga Burudani FC kwa bao 1-0.

Kocha wa Goms United Shabani Kazumba ‘Mourinho’ amesema alishaawambia watu tangu jana mechi yao ya leo angeimaliza ndani ya dakika 90 kama ilivyokuwa.

“Niliwaambia watu tangu jana nitamaliza mechi ndani ya dakika 90 namshukuru Mungu ametusaidia imekuwa hivyo. Maagizo niliyowapa wachezaji wameyatekeleza na ndio kimetupa ushindi,” Shabani Kazumba.

Kwa upande wa kocha wa Burudani Sultani Kipuga yeye amesema bahati ilikuwa kwa wapinzani wao kwa sababu vijana wake wamecheza vizuri.

“Sultani Kipuga wenzetu walituzidi bahati lakini uwezo tunafanana kabisa,” Sultani Kipuga.

Kuanzia hatua ya 16 bora, timu itakayoshinda mchezo wake itajipatia kitita cha shilingi 150,000 kutoka kwa kampuni ya Mcheza Tanzania wakati timu inayopoteza mechi inakabidhiwa shilingi 100,000 huku mchezaji bora wa mechi (man of the match akichukua shilingi 50,000.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here