Home Kimataifa Federer atwaa Wimbledon 2017

Federer atwaa Wimbledon 2017

1699
0
SHARE

Waswahili wanasema”mtoto mdogo halali na pesa” hicho ndio kilichomtokea Mcrotia  Marin Cilic ambaye leo alitarajia kuishangaza dunia katika fainali za Wimbledon.

Cilic amefungwa na Rodger Federer katika mchezo huo wa fainali na kumfanya Federer kushinda mashindano hayo kwa mara ya 8 na ikiwa Grand Slam yake ya 19.

Katika mchezo ambao ulichukua lisaa limoja tu na dakika 41 ilishuhudiwa Federer akiibuka kidedea kwa ushindi wa seti 6-3 6-1 na 6-4 dhidi ya Mcrotia huyo.

Federer amezidi kujikita kileleni kwa kuwa mcheza tennis mwenye makombe mengi zaidi na ushindi wa leo umemfanya kufikisha idadi ya makombe 19 makubwa.

Federer amevunja rekodi ya Bjorn Borg aliyoweka mwaka 1976 ya kushinda mashindano ya Wimblendon bila kupoteza seti hata moja katika mchezo huo.

Uzoefu ndio unaweza kuwa sababu ya Marin kupoteza fainali hiyo kwani hii ilikuwa fainali yake ya kwanza ya mashindano hayo huku ikiwa ya 11 kwa Rodger Federer.

Federer alikuwa na sababu nyingi za kummaliza Cilic kwani katika mchezo wa leo mkewe Mirka na watoto wao wakiwemo mapacha walikuwepo uwanjani kumpa suport baba yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here