Home Kimataifa Sio Conte na Costa pekee, wapo wengine waliowahi kuingia kwenye ‘bifu’ zito

Sio Conte na Costa pekee, wapo wengine waliowahi kuingia kwenye ‘bifu’ zito

6267
0
SHARE

Na Salym Juma, Arusha

Kuna taarifa zinaenea kwenye mitandao kumuhusu Antonio Conte kutaka kufanya mazungumza na Diego Costa ili waweze kumaliza tofauti zao ambazo zilitokea katikati ya msimu japokuwa Conte hakuzionesha hadharani. Nidhamu na kiburi vimehusika sana katika suala hili. Japo migogoro kati ya makocha na wachezaji sio suala geni katika nyanja ya michezo, leo hii tujaribu kutazama migogoro ya siku za karibuni iliyotokea kati ya wachezaji na makocha.

Pep Guardiola na Zlatan Ibrahimovic ni watu ambao hawakuwahi kuiva katika chungu kimoja. Ibrahimovic alisajiliwa kwa mbwembwe huku Eto’o akihusishwa katika usajili huu pamoja na Alexander Hleb.  “You bought a Ferrari, but you drive it like a Fiat” Haya ni baadhi ya maneno ya kejeli ambayo Zlatan amewahi kuyasema kwenye vyombo vya habari akimlenga Pep. Zlatan anadai hakuwahi kuzungumza na Pep tangu February 2010 hadi sasa.

Uhasama huu ulimfanya Zlatan kuondoka Barca kwani kwa madai yake ni kwamba Pep hakuwa anamtumia vile inavyopaswa. Messi alichagiza ‘bifu’ kwani Pep alionekana kumpenda zaidi mchezaji huyu katika nafasi ya mbele kuliko Zlatan. Hali ilimfanya Zlatan awachukie wawili hawa ambao wanapendana hadi kesho. Zlatan mara kadhaa amekuwa akidhihaki uwezo wa Pep huku Guardiola naye akidai Zlatan hana lolote uwanjani.

Iker Casillas na Jose Mourinho ni miongoni mwa wanasoka ambao waliwahi kuingia kwenye matatizo mazito. Mourinho alisitisha ufalme wa Casillas pale Santiago Bernabue kitu ambacho hakikuwaingia akilini Wana-Madrid. Antonio Adan alianzishwa badala ya Casillas na hapa ndipo ‘bifu’ lao lilipo shamiri. Diego Lopez alisajiliwa Madrid kwa lengo la kuzika utawala wa Iker. Mourinho hakuwahi kupendana na mlinda mlango huyu ambaye alikuwa kipenzi cha wengi.

Mourinho alipaswa kusuluhisha ugomvi kati ya Iker na CR7 ila ‘bifu’ lao lilishamiri baada ya Mou kuonekana kumchukia dhahiri Casillas ambaye amecheza mechi 700 akiwa Real Madrid. Usajili wa Iker kwenda Porto ulikuwa ni wa lazima kwani safari yake ya kubaki Madrid ilianza kuharibiwa na Mou. Casillas daima hawezi kuonekana mwema kwa Mou kutokana na wawili hawa kuwa katika ugomvi tangu Mou alivyotua Madrid.

Mario Balotelli na Brendan Rodgers hawakuwahi kuiva katika chungu kimoja japo wamefanya kazi muda mfupi sana pale Anfield. ‘Super Mario’ ni mchezaji mtukutu sana ambaye amekuwa akipishana na makocha wengi ila kwa Rodgers ilikuwa ‘Too much’ hadi kufikia hatua ya wao kutupiana maneno kwenye vyombo vya habari. Uhamisho wa Balotelli kuondoka Liverpool ulisababishwa na mahusino mabovu ya wawili hawa ambao wote kwa sasa hawapo Liverpool.

Carlos Tevez na Roberto Mancini pia walikumbwa na uhusiano mbovu kipindi ambacho wapo Manchester City. Tevez ni mchezaji mwenye kiburi ndiyo maana alishindwa kufanya kazi na Ferguson. Uhusiano wao uliharibiwa zaidi pale ambapo Mancin alimuamuru Tevezi ‘kupasha’ ili aingie kwenye mchezo dhidi ya Bayern ila kiburi cha Tevez kilisababisha agome kufanya hivyo jambo ambalo liliishangaza Dunia kwani tumezoea mambo haya kutokea Afrika.

Inawezekana ‘bifu’ lao lilianzia mbali hasa pale Mancin alipompoka kitambaa cha unahodha na kumpa Vicent Kompany. Tevez na Mancin inawezekana hadi sasa hawazungumzi kutokana na yaliyokuwa yanaendelea kati yao kwani huenda Mancin aliitafsiri vibaya hali iliyotokea kwenye mechi dhidi ya Bayern. Mancin amewahi kuingia matatani na Balotelli katika mazoezi ila wawili hawa walipatana lakini suala la Tevez haliwezi kumtoka kichwani hata mara moja.

Kuna wachezaji wengi wameingia katika mifarakano ya hapa na pale na makocha wao ila mwisho wa siku mahusiano yao yamekuja kuwa ya kawaida. David Bekham na Ferguson ni mfano mzuri, CR7 na Mou wamewahi kuingia katika mgogoro ila mwisho wa siku wanaonekana kuzungumza pamoja sehemu tofauti tofauti. Kupigwa benchi kwa baadhi ya wachezaji kumewafanya kuhusishwa na migogoro lakini mwisho wa siku hakuna kibaya kilichoendelea.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here