Home Kimataifa Japo umri unawatupa mkono, hawa ni wachezaji wanaozeeka na viwango vyao

Japo umri unawatupa mkono, hawa ni wachezaji wanaozeeka na viwango vyao

4932
0
SHARE

Na Salym Juma, Arusha

Kwenye mpira wa miguu, mchezaji akishafikisha miaka 30 huonekana mzee na hata kama akisajiliwa thamani yake kipesa huwa sio kubwa kama vijana wa miaka 22-28. Wachezaji wengi wakifikisha zaidi ya miaka 30 huonekana mizigo uwanjani na mara nyingi viwango vyao huporomoka na hili linadhihirika kila kukicha. Kwa baadhi ya wachezaji imekuwa tofauti kwani umri wao ni zaidi ya miaka 31 lakini viwango vyao bado vinahitajika kwenye timu na mashabiki wao.

Kutokana na hili, leo tuwatazame baadhi ya wachezaji ambao kiumri wanaonekana wazee ila kiuhalisia uwanjani wanaonekna bado vijana wadogo na ushahidi wa hili ulionekana msimu uliopita katika vilabu vyao.

Frank Ribéry ni winga wa Bayern Munich ambaye anaweza kunyumbulika upande wa kushoto au hata kulia kama kuna pengo. Ribery amehudumu Bayern kwa takribani miaka 10 tangu alipotoka Marseille mwaka 2007. Miaka 34 aliyonayo hivi sasa haitofautiani na winga wa miaka 23 anayecheza ‘Top flight league’. Msimu uliopita Frank aliisaidia Bayern kufika nusu fainali huku penati aliyokosa Vidal akiisababisha yeye. Ribery ni mfaransa ambaye amejijengea heshima Ujerumani.

Uwezo wake mkubwa umemfanya kuaminiwa na Ancelot japokuwa majeraha yamekuwa yakimuandama. Kiungo huyu mshambuliaji mwenye imani ya kiislamu amekuwa na misimu mizuri tangu ajiunge Bayern na ukweli ni kwamba namuona akizeeka na utamu wake uwanjani.

Arjen Robben ni mholanzi ambaye anajuta kuzaliwa kipindi ambacho dunia ina winga hatari kama Cristiano Ronaldo. Mchezaji huyu mwenye sura ya kizee ni ‘shida’ pindi anapokuwa na mpira. Robben anaweza kukugeuza anavyotaka, anakukimbiza vile anavyojiskia. Kwa sasa ana miaka 33, wachezaji alioanza nao karia wengi wamepotea ila yeye bado hajulikani ni lini ataanza kuanzia benchi. Chelsea ilimuuza kwenda Madrid ila ujio wa CR7 ulimfanya aende Bayern ambapo amechukua mataji yote.

Msimu uliomalizika alicheza michezo 37 na kufunga magoli 16 akiwa na klabu yake na kumfanya kuwa wa pili baada ya Lewandosk. Magoli 43 aliyoyafunga Roberto Lewandosk msimu uliomalizika yametokana na usumbufu wa winga huyu ambaye amechukua vikombe vyote isipokuwa World Cup.

Andres Iniesta ni kiungo mchezeshaji wa FC Barcelona. Wakati mwingine unapata kigugumizi kusema eti Messi na CR7 ndio wachezaji bora wa Dunia tangu 2008 hadi sasa. Iniesta anastahili kuitwa fundi wa mpira japokuwa hadi sasa ana miaka takriban 33. Msimu uliomalizika aliisaidia Barca japokuwa Barca walishindwa kujisaidia wenyewe. Amejaaliwa nidhamu na kipaji cha hali juu hasa katika kupiga pasi. Messi anafurahia uwepo wa Iniesta na huenda anatamani Iniesta azidi kuwa kama sasa.

Msimu uliomalizika Iniesta alicheza michezo 37, japokuwa umri umekwenda uwezo wake ulikwa ni kama wa kiungo ‘mbichi’ wa miaka 20. Naweza kusema kwa kujiamini kuwa huyu jamaa huenda akastaafu na utamu wake kama ‘Pacha’ wake Xavi Hernandez ambaye Lamasia inam-msi hadi sasa.

Cristiano Ronaldo ni moja kati ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika zama hizi. Nikisema CR7 analijua goli kuliko mchezaji yoyote sizani kama nitakuwa nakosea japo nakuruhusu unikosoe. Katika michezo 265 aliyoichezea Madrid, CR7 amefunga magoli 285. Kwa sasa anaelekea mwaka wa 33 ila akiwa kwenye kumi na nane za wapinzani, CR7 amekuwa ‘Clinical finisher’ mzuri na hili lilidhihirika kwenye ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita kutokana na ‘hat-trick’ alizopiga.

Msimu uliomalizika CR7 alicheza mechi 46 na kufunga magoli 42 huku akiisaidia Madrid kushinda taji la 12 la UEFA na ubingwa wa La liga pia. Ronaldo hawezi kupiga tena mikasi au kukimbia kwa kasi ila hajazeeka kwenye ufungaji. CR7 naweza kusema anazeeka na utamu wake wa ufungaji.

Dani Alves ni beki wa kulia aliyezaliwa nchini Brazil miaka 34 iliyopita. Kwa sasa amesajiliwa na matajiri wa PSG akitokea Juventus kama mchezaji huru. Barca hadi kesho itawachukua muda mrefu kumpata beki wa kulia mwenye sifa kama za Alves. Uwezo wake wa kupanda na kushuka hautofautiani na Marcelo anayecheza kushoto pale Madrid. Baada ya kuondoka Barca, Juventus walifurahia huduma yake licha ya umri wake kuwa mkubwa. Dani Alves haendani kabisa na umri wake.

Msimu uliomalizika Alves aliichezea Juventus michezo 33 na kufunga magoli 6. Man City wamejaribu mara kadhaa kumsajili ila PSG waliwazidi kete. Alves anazeeka na ufundi wake kwani kasi yake haitofautiani na ile ya 2010.

latan Ibrahmovich ni Mshambuliaji hatari ambaye amekamilika. Zlatan kacheza katika vilabu vikubwa barani Ulaya kwa kiwango cha juu. Msimu uliopita Kadabra aliwabeba Mashetani wekundu na lau kama majeraha yasingemuandama huenda angefunga zaidi ya magoli aliyokuwa nayo. Japokuwa Man United wamemuacha kwenye usajili ila kilichosababisha ni majeraha na sio kiwango. Miaka aliyonayo Mshambuliaji huyu haiendani na kiwango chake kabisa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here