Home Kimataifa Tetesi za usajili majuu hii leo, Madrid wapiga hodi tena United

Tetesi za usajili majuu hii leo, Madrid wapiga hodi tena United

8111
0
SHARE

Beki kisiki wa klabu ya Juventus Leornado Bonucci ameachana na klabu hiyo na sasa anakwenda kujiunga na klabu ya Ac Millan ya nchini humo Italia kwa uhamisho ulioigharimu Ac Millan kiasi cha £35.2m.

Klabu ya RB Leizpg imeendelea kuiwekea ngumu klabu ya Liverpool kwani baada ya ada ya mwanzo ya Liverpool ya £35m kukataliwa, Liverpool walituma ofa nyingine ya £50m ambayo nayo imekataliwa.

Klabu ya Real Madrid imepiga hodi tena katika klabu ya Manchester United, Madrid wamekuja tena na ofa kubwa zaidi kumnyakua mlinda mlango David De Gea na taarifa zinadai United wameanza kushawishika kwa dau hilo.

Klabu za Chelsea na Juventus zimejikuta zikiingia vitani kuwania sahihi ya mlinzi wa kulia wa klabu ya Real Madrid Danilo ambaye dalili zote zinaonesha anaweza kuondoka Santiago Bernabeu majira haya.

Katika kile kinachoonesha kupania kurudisha heshima inayoonekana kushuka, kocha Pep Gurdiola ametuma ofa ya  kiasi cha £90 kwa ajili ya usajili wa Tottenham Kyle Walker na taarifa zinasema mlinzi huyo atakuwepo kwenye kikosi cha City kinachoenda Marekani.

Wakati huo huo City wakikamilisha usajili wa mlinzi huyo wa kulia wa Tottenham lakini poa taarifa zinadai uhamisho wa mlinzi wa kushoto wa Monaco Benjamin Mendy kwenda Man City uko katika hatua za mwisho mwisho.

Kama United wakishindwa kumsajili kiungo wa Tottenham Hotspur Eric Dier baasi watarudi tena As Roma kujaribu kumnunua Raja Nainggolan ambaye thamani yake ni £40m.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here