Home Kitaifa Singano: Mimi Sio Star, Nakwenda Kupambana Morocco

Singano: Mimi Sio Star, Nakwenda Kupambana Morocco

4205
0
SHARE

Na  Zainabu Rajabu

KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano, ameondoka nchini leo kwenda Morocco kujiunga na timu ya Difaâ Hassani d’ El Jadida inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Singano ambaye alijiunga na Azam misimu miwili iliyopita akitokea Simba, anakwenda kujiunga na timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na Azam.

Shaffidauda.co.tz imezungumza na Singano akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kupanda ndege.

Singano anaanza kwa kusema: “Naushukuru uongozi wa klabu yangu ya Azam kwa kuniruhusu kwani tulikaa na kukubaliana kuhusu suala langu hili la safari.

SWALI: Ulipataje dili hili

JIBU: Tunapocheza, kikubwa timu nyingi huwa zinatufuatilia, hivyo nadhani waliniona wakati nacheza na timu yangu ya Azam.

SWALI: Unaenda kusaini mkataba wa muda gani?

JIBU: Mkataba ninaokwenda kusaini ni siri ya mchezaji na klabu husika.

SWALI: Ushawahi kuifuatilia Ligi ya Morocco?

JIBU: Kiukweli ninapokuwa nyumbani huwa nafuatilia sana ligi mbalimbali, kikubwa nilipojua nakwenda nchi hiyo nikaanza kuifuatilia. Niwaombe Watanzania waniombee dua niweze kufikia malengo yangu.

SWALI: Tumeona mastaa wengi wa Azam wakiondoka kipindi hiki huku sababu kubwa ikitajwa ni sera ya kubana matumizi ndiyo inayowakimbiza, kwako ikoje?

JIBU: Mimi bado sijawa staa kama wengine, lakini hilo la wachezaji kuondoka kila mmoja na muono wake.

Binafsi baada ya kuona nimecheza takribani misimu kama minne hapa nyumbani nikaona kwa nini nisitafute changamoto nyingine nje ya Tanzania, ndio ikatokea hii, kikubwa nakwenda kupambana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here