Home Kimataifa Bolasie ajipa moyo kuhusu kurudi uwanjani na ujio wa Wazza

Bolasie ajipa moyo kuhusu kurudi uwanjani na ujio wa Wazza

3479
0
SHARE

Klabu ya Everton ilikuwepo nchini Tanzania tangu siku ya Jumatano na jana siku ya Alhamisi walicheza mchezo wa kujiandaa na ligi kuu Uingereza dhidi ya klabu ya Gormahia ya nchini Kenya.

Wachezaji wengi wakubwa akiwemo Wayne Rooney walikuwepo uwanjani katika mchezo huo uliomalizika kwa Everton kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja lakini Mkongomani Yannick Bolasie alikuwa nje.

Tangu kuwasili kwa Everton nchini Tanzania mchezaji huyo alionekana akiwa amekaa peke yake nje wakati wenzie wakifanya mazoezi hali inayoashiria kwamba bado anaugulia maumivu aliyoyapata mwezi December mwaka jana.

Bolasie amesema bado hali yake sio nzuri sana kwa kuanza mazoezi na hataonekana katika mwanzo wa msimu ujao wa Epl lakini amesisitiza kwamba anaamini kabla raundi ya kwanza ya Epl haijamalizika anaweza kurejea uwanjani.

Kuhusu ujio wa  Rooney alisema “ni usajili mzuri sana kwetu na naamini utaleta changamoto mpya katika ushindani wa namba lakini mimi kama mchezaji nahitaji changamoto ili kukuza kiwango changu”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here