Home Kitaifa Mwashiuya Amlilia Niyonzima

Mwashiuya Amlilia Niyonzima

12452
0
SHARE
Winga wa Yanga Godfrey Mwashiuya akiruka kwanja la beki wa Azam FC Agrey Morris wakati wa mchezo wao wa robofainali

Na Zainabu Rajabu

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya ameonesha hisia zake kali mara baada ya kubaini kwamba mchezaji mwenzake Haruna Niyonzima hatakuwepo katika kikosi chao msimu ujao.

Niyonzima ambaye ametajwa kusajiliwa na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili, anaachana na Yanga mara baada ya kumaliza mkataba wake msimu uliopita kumalizika.

Shaffidauda.co.tz ilitembelea  kwenye mitandao ya kijamii na kushuhudia  baadhi ya wachezaji wa Yanga wakionesha hisia zao kuhusu kuondoka kwa  kiungo huyo mahariri katika kikosi chao.

Haya ni maneno ya Mwashiuya akimpa maneno ya kwa heri Niyonzima na kumtakia maisha mema katika timu yake mpya.

“Pengo kubwa  sana, dah nenda bro wangu Mungu akupe mafanikio mema huko uendako, nakukubali sana chaboli”.

Niyonzima anaondoka akiwa bado ana deni kubwa sana kwa Wana Yanga ambao walikuwa wanaona kama ndiyo mtu ambae alikuwa anajua nini anafanya awapo uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here