Home Dauda TV Video: Star wa Everton amepata mapokezi makubwa Tanzania kutoka kwa raia wa...

Video: Star wa Everton amepata mapokezi makubwa Tanzania kutoka kwa raia wa DR Congo

7360
0
SHARE

Mashabiki wengi raia wa DR Congo walijitokeza ku-show love kwa mchezaji Yannick Bolasie anaecheza Everton na timu yataifa ya Congo wakati akiwasili Tanzania na kikosi kizima cha Everton kwa ajili ya mechi yao ya kirafiki ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi ya England.

Wakiwa wamevalia t-shirts zenye picha ya Bolasie, wameshika bendera za taifa lao walikuwa wakicheza na kuimba jina la mkali huyo.

Dauda TV ilipata fursa ya kuzungumza na mmoja kati ya mashabiki hao ambaye amesema wanajisikia faraja na fahari kumuona mchezaji wao akiiwakilisha nchi yao kwenye ligi kubwa na pia kupata fursa ya kumshuhudia katika kikosi cha Everton kilichokuja Tanzania kwa ziara ya pre-season.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here