Home Kimataifa Picha 8: Rooney alivyotua Tanzania na kikosi cha Everton

Picha 8: Rooney alivyotua Tanzania na kikosi cha Everton

10654
0
SHARE

Wayne Rooney amewasili kwenye ardhi ya Bongo akiwa na kikosi kizima cha Everton kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi ya England.

Everton watacheza kesho na Gor Mahia kwenye uwanja wa taifa, Gor Mahia wamepata fursa ya kucheza na Everton baada ya kuwa washindi wa SportPesa Super Cup mashindano yaliyoshirikisha timu zote zinazodhaminiwa na kampuni ya SportPesa.

Mastaa wengine walioambatana kikosi cha Everton ni pamoja ba Aron Lennon, Yannick Bolasie ambaye ni raia wa DR Congo, Michael Kane, Phil Jagielka, Morgan Schneiderlin pamoja na kocha mkuu wa klabu hiyo Ronald Koeman.

Mbali na mechi ya kirafiki dhidi Gor Mahia, Everton pia watafanya shughuli nyingine ikiwemo kutembelea Shule ya Msingi Uhuru, wataendesha pia clinic ya soccer Gymkhana.

Jambo la kuvutia baada ya Everton kutua Tanzania ilikua ni uwepo wa mashabiki wengi wenye asili ya DR Congo ambao walijitokeza kum-support Bolasie.

Waziri mwenye dhamana ya Michezo nchini, Dkt. Harrison Mwakyembe alikuwepo uwanja wa ndege kwa ajili ya kuwapokea wachezaji wa Everton.

Hii ni fursa pekee iliyoletwa na SportPesa kwa wapenzi wa soka Tanzania kuishuhudia timu hiyo ikicheza uwanja wa taifa pamoja na kuwashuhudia mastaa wengi wanaofanya vizuri kwenye ligi kuu ya England.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here