Home Kitaifa Mtibwa Sugar kuweka kambi Dar.

Mtibwa Sugar kuweka kambi Dar.

2089
0
SHARE
Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakipongezana baada ya Jaffar Kibaya kuifungia Mtibwa bao la pili dhidi ya African Sports

Na Zainabu Rajabu.

TIMU ya Mtibwa Sugar itapiga kambi ya wiki mbili jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara utakaoanza mwishoni mwa Agosti.

Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru  akizungumza na Shaffidauda.co.tz. alisema kambi hiyo itaanza Jumatano  na wanaamini itawasaidia kufanya vizuri kwenye msimu ujao wa ligi.

Kifaru alisema kwa asilimia kubwa wamemaliza usajili wao mabao wameufanya kwa umakini hasa kwa kusajili vijana ambao wanaamini wataipa mafanikio klabu hiyo.

“Tutaweka kambi ya mazoezi kwa wiki mbili Dar es Salaam  mpaka Julai 28  na Julai 29 tutacheza mchezo wa kuwania kombe la  Faith Baptist  dhidi ya Mbeya City  utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri  Morogoro na baada ya mchezo huo tutarejea Turiani kuendelea na kambi,”alisema Kifaru.

Msemaji huyo alisema  baada ya wachezaji kadhaa kuondoka katika timu hiyo akiwemo beki Salim Mbonde na winga Ally Shomari waliotimkia Simba wamewaongeza wachezaji vijana kuziba nafasi zao wakiwemo Hassan Iddi kutoka  Oljoro JKT na  Salum Ramadhan  kutoka Polisi Morogoro.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here