Home Kitaifa Kotei Aongeza Mkataba Mpya Simba Sc.

Kotei Aongeza Mkataba Mpya Simba Sc.

3875
0
SHARE

Na Zainabu Rajabu.

Kiungo wa kimataifa wa Ghana James Kotei ameongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kuichezea Klabu ya Simba.

Kotei alisajiliwa na Simba Kwenye dirisha dogo msimu uliopita kuchukua nafasi ya Mussa Ndusha.

Kotei ambaye ana uwezo pia wa kucheza nafasi ya beki wa kati, leo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope ameongeza mkataba wa miaka miwili.

Kuongeza mkataba kwa kiungo huyo, kunazima tetesi za yeye kutakiwa na mahasimu wakubwa wa Simba, Klabu ya Yanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here