Home Dauda TV Video: Singida United imetambulisha wachezaji wawili kutoka Rwanda

Video: Singida United imetambulisha wachezaji wawili kutoka Rwanda

3592
0
SHARE

Singida United imetambulisha wachezaji wengine wawili wa kimataifa Michel Rusheshangoga na Danny Usengimana wote raia wa Rwanda na wachezaji wa timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’.

Michel beki wa kulia amesajiliwa kutoka APR ambako alikuwa nahodha wa kikosi hicho, Usengimana yeye ni mshambuliaji na alikuwa akicheza kwenye kikosi cha Police FC huku akiwa ni mfungaji bora wa ligi ya Rwanda kwa misimu miwili mfululizo (2015/16 na 2016/17).

Michel Rusheshangoga

Wawili hao wametua Dar leo Julai 11, 2017 wakitokea Rwanda na kupokelewa na Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga. Michel na Usengimana wameunganisha moja kwa moja jijini mwanza kuungana na kikosi cha Singida United ambacho kipo kambini kikijiandaa na msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

Danny Usengimana

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here